Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mhubiri 6:4-9 in Swahili (individual language)

Help us?

Mhubiri 6:4-9 in Biblia ya Kiswahili

4 Hata mtoto huyo amezaliwa bila faida na anapita katika giza, na jina lake linabaki limefichika.
5 Ingawa mtoto huyu haoni jua au kujua kitu chochote, ana pumziko ingawa mtu huyo hakupumzika.
6 Hata kama mtu akiishi miaka elfu mbili lakini hajifunzi kufuraia vitu vizuri, aenda sehemu moja kama mtu yeyote yule.
7 Ingawa kazi yote ya mtu ni kujaza mdomo wake, ila hamu yake haishibi.
8 Hakika ni faida gani aliyo nayo mwenye hekima kuliko mpumbavu? Ni faida gani aliyo nayo masikini hata kama anajua jinsi ya kutenda mbele ya watu?
9 Ni bora kuridhika na kile ambacho macho hukiona kuliko kutamani kile ambacho hamu isiyo tulia inatamani, ambayo pia ni mvuke na kujaribu kuuchunga upepo.
Mhubiri 6 in Biblia ya Kiswahili