Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mhubiri 5:4-16 in Swahili (individual language)

Help us?

Mhubiri 5:4-16 in Biblia ya Kiswahili

4 Ukiweka nadhili kwa Mungu, usichelewe kuifanya, kwa kuwa Mungu hafurahii upumbavu. Fanya kile ulichoapa utakifanya.
5 Ni bora kutokuweka nadhiri kuliko kuweka nadhiri ambayo usiyoiondoa.
6 Usiuruhusu mdomo wako kusababisha mwili wako kutenda dhambi. Usiseme kwa mtumwa wa kuhani, “Kile kiapo kilikuwa kwa makosa.” Kwani nini kumfanya Mungu akasirike kwa kuapa kwa uongo, kumchochea Mungu aharibu kazi ya mikono yako?
7 Kwa kuwa katika ndoto nyingi, kama ilivyo katika maneno mengi, kuna mvuke ubatili. Hivyo mwogope Mungu.
8 Unapomwona masikini akiteswa na kunyang'anywa haki na kutendewa vibaya katika jimbo lako, usishangae kama kwamba hakuna anaye fahamu, kwa sababu kuna watu katika mamlaka ambao hutazama, kuna hata walio juu yao.
9 Kwa nyongeza uzalishaji wa ardhi ni kwa kila mmoja, na mfalme mwenyewe huchukua uzalishaji kutoka mashambani.
10 Yeyote apendaye fedha hatatosheka na fedha, na yeyote apendaye utajiri mara zote hutaka zaidi. Huu pia ni mvuke.
11 Kadri mafanikio yanapoongezeka, ndivyo wanavyoongezeka watu wanaotumia. Kuna faida gani katika utajiri kwa mmiliki isipokuwa kuutazama kwa macho yake?
12 Usingizi wa mfanyakazi ni mtamu, kama anakula kidogo au sana, lakini utajiri wa mtu tajiri haumuruhusu yeye kulala vizuri.
13 Kuna jambo baya zaidi ambalo nimeliona chini ya jua: mali iliyowekwa akiba na mwenye nayo, inamsababishia taabu mwenyewe.
14 Wakati tajiri anapopoteza utajiri wake kwa bahati mbaya, mwana wake, ambaye amemzaa, habakiziwi chochote mikononi mwake.
15 Kama mtu azaliwavyo uchi kutoka tumboni mwa mamaye, vivyo hivyo ataondoka katika maisha haya akiwa uchi. Hachukui chochote kutoka katika kazi yake.
16 Jambo jingine baya kabisa, kama mtu alivyo kuja ni lazima aende vivyo hivyo. Hivyo ni faida gani mtu yeyote aipatayo katika kufanya kwa ajili ya upepo?
Mhubiri 5 in Biblia ya Kiswahili