Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mhubiri 3:8-17 in Swahili (individual language)

Help us?

Mhubiri 3:8-17 in Biblia ya Kiswahili

8 Kuna wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia, wakati wa vita na wakati wa amani.
9 Ni faida gani mfanyakazi aipatayo katika kazi yake?
10 Nimeona kazi ambayo Mungu amewapa wanadamu kuitimiza.
11 Mungu amefanya kila kitu kufaa kwa wakati wake. Pia ameweka umilele ndani ya mioyo yao. Lakini mwanadamu hawezi kuelewa matendo ambayo Mungu ameyafanya, tangu mwanzo wao hadi mwisho.
12 Ninajua kuwa hakuna kilicho bora kwa mtu yeyote kuliko kufurahi na kutenda mema maadamu anaishi-
13 na kwamba kila mmoja anapaswa ale na kunywa na anapaswa kuelewa jinsi ya kufurahia mazuri ambayo yanatoka katika kazi zake zote. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu.
14 Ninajua kwamba chochote afanyacho Mungu kinadumu milele. Hakuna kinaweza kuongezwa au kuondolea, kwa sababu Mungu ndiye aliyekifanya, ili kwamba watu wamsogelee kwa heshima.
15 Chochote kilichopo kimekwisha kuwepo; chochote kitakachokuwepo kimekwisha kuwepo. Mungu huwafanya wanadamu kutafuka vitu vilivyjificha.
16 Na nimeona kwamba chini ya jua ubaya upo mahali palipopaswa kuwa na haki, na sehemu ya haki mara nyingi ina ubaya.
17 Nikasema moyoni mwangu, “Mungu atahukumu mwenye haki na mbaya kwa wakati muafaka kwa kila jambo na kila tendo.
Mhubiri 3 in Biblia ya Kiswahili