Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mhubiri 3:12-21 in Swahili (individual language)

Help us?

Mhubiri 3:12-21 in Biblia ya Kiswahili

12 Ninajua kuwa hakuna kilicho bora kwa mtu yeyote kuliko kufurahi na kutenda mema maadamu anaishi-
13 na kwamba kila mmoja anapaswa ale na kunywa na anapaswa kuelewa jinsi ya kufurahia mazuri ambayo yanatoka katika kazi zake zote. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu.
14 Ninajua kwamba chochote afanyacho Mungu kinadumu milele. Hakuna kinaweza kuongezwa au kuondolea, kwa sababu Mungu ndiye aliyekifanya, ili kwamba watu wamsogelee kwa heshima.
15 Chochote kilichopo kimekwisha kuwepo; chochote kitakachokuwepo kimekwisha kuwepo. Mungu huwafanya wanadamu kutafuka vitu vilivyjificha.
16 Na nimeona kwamba chini ya jua ubaya upo mahali palipopaswa kuwa na haki, na sehemu ya haki mara nyingi ina ubaya.
17 Nikasema moyoni mwangu, “Mungu atahukumu mwenye haki na mbaya kwa wakati muafaka kwa kila jambo na kila tendo.
18 Nikasema moyoni mwangu, “Mungu huwajaribu wanadamu kuwaonyesha kwamba wao ni kama wanyama.”
19 Kwa kuwa mwisho watoto wa wanadamu na mwisho wa wanyama ni sawa. Kifo cha mmoja ni sawa na kifo cha mwingine. Wote wana pumzi sawa. Hakuna faida kwa mwanadamu zaidi ya wanyama. Kwa kuwa hakuna kila kitu isipokuwa pumzi?
20 Kila kitu kinaenda sehemu moja. Kila kitu kinatoka mavumbini, na kila kitu kinarudi katika mavumbini.
21 Ni nani ajuaye kama roho ya mwanadamu inaenda juu na roho ya wanyama inaenda chini ya nchi?
Mhubiri 3 in Biblia ya Kiswahili