13 Kisha nikaanza kuelewa kwamba hekima ina faida kuliko upumbavu, kama nuru ilivyo bora kuliko giza.
14 Mwenye hekima hutumia macho yake katika kichwa chake kuona mahali anakoenda, lakini mpumbavu hutembea katika giza, ingawa ninafahamu kuwa mwisho wa aina moja umetunzwa kwa kila mmoja.
15 Kisha nikasema moyoni mwangu, “Kinachotokea kwa mpumbavu, ndicho kitachotokea na kwangu. Hivyo kuna utofauti gani kama mimi ni mwenye hekima sana?” Nikahitimisha moyoni mwangu, “Huu pia ni mvuke tu.”
16 Kwa kuwa mwenye hekima, kama mpumbavu, hakumbukwi kwa muda mrefu. Katika siku zijazo, kila kitu kitakuwa kimesahauliwa. Mwenye hekima hufa kama navyokufa mpumbavu.
17 Hivyo nikauchukia uhai kwa sababu kazi zote zilizofanyika chini ya jua zilikuwa mbaya kwangu. Hii ni kwa sababu kila kitu ni mvuke na kujaribu kuuchunga upepo.
18 Nikachukia yote niliyoyatimiza, ambayo nilikuwa nimekwisha yafanya chini ya jua kwa sababu ni lazima niyaache kwa mtu anaye kuja baada yangu.
19 Na ni nani ajuaye kama atakuwa mwenye hekima au mpumbavu? Ila atakuwa msimamizi juu ya kila kitu chini ya jua ambayo kazi yangu na hekima yangu imeyajenga. Huu pia ni mvuke.
20 Kwa hiyo moyo wangu ukaanza kukata tamaa juu ya kazi zote nilizozifanya chini ya jua.