Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mambo ya Walawi 7:9-19 in Swahili (individual language)

Help us?

Mambo ya Walawi 7:9-19 in Biblia ya Kiswahili

9 Kila sadaka ya nafaka inayookwa mekoni, na kila sadaka kama hiyo ipikwayo kaangoni au kwenye sufuria itakuwa ya kuhani aitoaye.
10 Kila sadaka ya nafaka, ama iwe unga mkavu au uliochanganywa na mafuta ya zeitu itakuwa ya ukoo wa Aroni kwa usawa.
11 Hii ndiyo sheria ya dhabihu ya sadaka za amani, ambazo watu watazitoa kwa Yahweh.
12 Iwapo mtu yeyote anaitoa ili kuonyesha shukrani kwa Yahweh, basi ataitoa pamoja na dhabih uya mikate iliyotengenezwa bila hamira, bali kwa mafuta ya zeituni yaliyochanganywa na unga lakini bila hamira, na maandazi yaliyotengenezwa bila hamira, bali yaliyopakwa mafuta juu yake, na mikate miembamba iliyofanywa kwa unga laini uliochanganywa na mafuta.
13 Kwa kusudi la kutoa shukrani, pia anapaswa kutoa pamoja na sadaka yake ya amani, vipande vya mikate iliyotiwa hamira.
14 Ni lazima atatoa moja kila aina ya sadaka hizi kama sadaka iliyoletwa kwa Yahweh. Nayo itakuwa ya makuhani wanaonyunyizia damu ya sadaka ya amani kwenye madhabahu.
15 Mtu anayeleta sadaka ya amani kwa kusudi la kutoa shukrani ni lazima ataila nyama ya sadaka yake siku ya kutoa dhabihu. Hatakiwi kusaza chochote kilicho cha sadaka hiyo hata asubuhi ya pili.
16 Lakini iwapo dhabihu ya matoleo yake kusudi lake ni nadhiri, au kwa kusudi la sadaka ya hiari, nyama yake italiwa siku iyo hiyo aitoapo dhabihu yake, lakini chochote kinachosalia cha sadaka hiyo kinaweza kuliwa siku inayofuata.
17 Hata hivyo, nyama yoyote ya dhabihu inayobaki siku ya tatu ni lazima ichomwe moto.
18 Iwapo kipande chochote cha nyama hiyo ya dhabihu kinachobaki kinaliwa katika siku ya tatu, hakitakubalika, wala hakitatolewa kwa aliyeitoa. Kitakuwa ni kitu cha kuchukiza, na mtu akilaye atabeba hatia ya dhambi mwenyewe yake.
19 Nyama yoyote inayogusa kitu kilicho najisi haitaliwa. Ni lazima ichomwe moto. Na kwa ajili ya nyama inayobaki, yeyote aliye safi anaweza kuila.
Mambo ya Walawi 7 in Biblia ya Kiswahili