Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mambo ya Walawi 7:23-31 in Swahili (individual language)

Help us?

Mambo ya Walawi 7:23-31 in Biblia ya Kiswahili

23 “Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, 'hamruhusiwi kula mafuta ya fahali au kondoo au mbuzi.
24 Mafuta ya mnyama yoyote afaye peke yake bila ya kuwa dhabihu, au mafuta ya mnyama yeyote aliyeraruliwa na wanyama pori, yanaweza kutumika kwa makusudi mengine, lakini hakika hamtayala.
25 Yeyote atakayekula mafuta ya mnyama ambayo watu wanaweza kuyatoa kuwa dhabihu ya iliyofanywa kwa Yahweh kwa moto, mtu huyo lazima atakatiliwa mbali kutoka kwa watu wake.
26 Hamtakula damu yoyote katika mojawapo ya nyumba zenu, ama iwe kutoka kwa ndege au mnyama.
27 Yeyote alaye damu yoyote, mtu huyo lazima akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.'”
28 Kwa hiyo Yahweh akazungumza na Musa na akasema,
29 “Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, 'Yeye atoaye dhabidhu ya sadaka ya amani kwa Yahweh lazima alete sehemu ya dhabihu yake kwa Yahweh.
30 Mikono yake mwenyewe lazima iilete hiyo sadaka ifanywayo kwa Yahweh kwa moto. Naye atayaleta hayo mafuta pamoja na kidari, ili kwamba kidari kiweze kutikiswa kuwa sadaka ya kutikiswa mbele za Yahweh.
31 Kuhani atayachoma mafuta hayo juu ya madhabahu, lakini kile kidari kitakuwa mali ya Aroni na uzao wake.
Mambo ya Walawi 7 in Biblia ya Kiswahili