Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mambo ya Walawi 7:21-29 in Swahili (individual language)

Help us?

Mambo ya Walawi 7:21-29 in Biblia ya Kiswahili

21 Iwapo mtu yeyote anagusa kitu chochote kilichonajisi—iwe ni unajisi wa binadamu, au wa mnyama aliyenajisi, au wa kitu fulani kilichonajisi na chenye kuchukiza, na kisha akala baadhi ya nyama ya dhabihu ya sadaka ya amani iliyotolewa kwa Yahweh, lazima mtu huyo akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.
22 Kisha Yahweh akazungumza na Musa, akisema,
23 “Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, 'hamruhusiwi kula mafuta ya fahali au kondoo au mbuzi.
24 Mafuta ya mnyama yoyote afaye peke yake bila ya kuwa dhabihu, au mafuta ya mnyama yeyote aliyeraruliwa na wanyama pori, yanaweza kutumika kwa makusudi mengine, lakini hakika hamtayala.
25 Yeyote atakayekula mafuta ya mnyama ambayo watu wanaweza kuyatoa kuwa dhabihu ya iliyofanywa kwa Yahweh kwa moto, mtu huyo lazima atakatiliwa mbali kutoka kwa watu wake.
26 Hamtakula damu yoyote katika mojawapo ya nyumba zenu, ama iwe kutoka kwa ndege au mnyama.
27 Yeyote alaye damu yoyote, mtu huyo lazima akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.'”
28 Kwa hiyo Yahweh akazungumza na Musa na akasema,
29 “Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, 'Yeye atoaye dhabidhu ya sadaka ya amani kwa Yahweh lazima alete sehemu ya dhabihu yake kwa Yahweh.
Mambo ya Walawi 7 in Biblia ya Kiswahili