Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mambo ya Walawi 6:7-21 in Swahili (individual language)

Help us?

Mambo ya Walawi 6:7-21 in Biblia ya Kiswahili

7 Kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele ya Bwana, atakuwa amesamehewa kulingana na chochote kilicho mfanya kuwa na hatia.”
8 Ndipo Bwana alisema na Musa kumwambia,
9 “Mwagize Haruni na wanawe, kusema, 'hii ni sheria ya sadaka ya kuteketezwa: Sadaka ya kuteketezwa lazima iwe juu ya makaa ya madhabahu usiku wote hata asubuhi, na moto wa madhabahu utaendelea kuwaka.
10 Kuhani atavaa nguo zake za kitani na atavaa nguo za kitani ndani yake. Atatoa majivu yaliyobaki baada ya moto kutekeza sadaka ya kuteketezwa juu ya madhabahu, na ataweka majivu pembeni mwa madhabahu.
11 Atavua mavazi haya na kuvaa mavazi mengine ili kuchukua majivu nje ya kambi na kupeleka mahali palipo safi.
12 Moto katika madhabahu utaendelea kuwaka. Usizimike, na kuhani ataongeza kuni kila asubuhi. Atapanga juu yake sadaka ya kuteketezwa kama inavyotakiwa, na atateketeza juu yake mafuta ya sadaka ya amani.
13 Moto lazima utaendelea kuwaka katika madhabahu, kamwe usizimike.
14 Hii ni sheria ya sadaka ya nafaka. Wana wa Haruni watatoa mbele ya Bwana katika madhabahu.
15 Kuhani atachukua konzi ya unga laini wa sadaka ya nafaka na mafuta na ubani ambao uko juu ya sadaka ya nafaka, atateketeza juu ya madhabahu kuleta harufu nzuri ya shukrani ya kumpendeza Bwana.
16 Haruni na wanae watakula sadaka inayobaki, italiwa bila kutiwa chachu mahali patakatifu. Watakula katika ua ya hema ya kukutania.
17 Haitaokwa pamoja na chachu. Nimewapa kama sehemu ya sadaka yangu itolewayo kwa moto, ni takatifu sana, kama sadaka ya dhambi na sadaka ya hatia.
18 Kwa nyakati zote zijazo kupitia watu wa kizazi chako, mwanaume yeyote mzaliwa kutoka kwa Haruni aweza kula ni sehemu yake, ichukuliwayo katika sadaka ya Bwana kwa moto. Yeyote anayeigusa atakuwa mtakatifu.”
19 Bwana aliongea tena na Musa kumwambia,
20 “Hii ni sadaka ya Haruni na wanawe ambayo watatoa kwa Bwana katika siku ambayo kila mwana atawekwa wakfu: sehemu ya kumi ya efa ya unga laini kama kawaida sadaka ya nafaka nusu yake asubuhi na nusu yake jioni.
21 Itatengenezwa na mafuta katika kikaango, utaileta ikiwa imeandaliwa imeokwa katika vipande utatoa sadaka ya nafaka ili kuleta harufu nzuri kwa Bwana.
Mambo ya Walawi 6 in Biblia ya Kiswahili