Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mambo ya Walawi 5:8-14 in Swahili (individual language)

Help us?

Mambo ya Walawi 5:8-14 in Biblia ya Kiswahili

8 Atawaleta kwa kuhani, wa kwanza atatoa kwa ajili ya sadaka ya dhambi. Atamvunja shingo yake lakini ataacha kichwa chake kinaning'inia wala hataiondoa kabisa shingo yake katika mwili.
9 Ndipo atanyunyizia damu yake katika sehemu za madhabahu, na damu inayobaki ataimwaga chini ya madhabahu. Hii ni dhabihu ya dhambi.
10 Ndipo ataoa ndege wa pili kama sadaka ya kuteketezwa kama ilivyoelekezwa, na kuhani atafanya upatanisho kwa ajili ya dhambi alizokwisha kufanya, na huyo mtu atakuwa amesamehewa.
11 Lakini kama hataweza kununua hua wawili au makinda ya njiwa mawili, ndipo ataleta kama dhabihu ya dhambi zake sehemu ya kumi ya unga laini kama sadaka ya dhambi. Asiweke mafuta wala ubani juu yake, kwa kuwa ni sadaka ya dhambi.
12 Atauleta kwa kuhani, na kuhani atachukua konzi moja ya unga kama ukumbusho wa wema wa Bwana na atauweka juu ya madhabahu na kuteketeza juu ya sadaka za kuteketezwa kwa moto kwa ajili ya Bwana. Hii ni sadaka ya dhambi.
13 Kuhani atafanya upatanisho kwa dhambi yoyote aliyofanya mtu yeyote, mtu huyo atasamehewa. Na sadaka inayobaki itakuwa ya kuhani, kama ilivyo sadaka ya nafaka.'”
14 Bwana akamwambia Musa, akasema,
Mambo ya Walawi 5 in Biblia ya Kiswahili