Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mambo ya Walawi 4:20-35 in Swahili (individual language)

Help us?

Mambo ya Walawi 4:20-35 in Biblia ya Kiswahili

20 Hivyo ndivyo atakavyomfanya huyo ng'ombe, kama alivyomfanya ng'ombe wa sadaka ya dhambi, atamfanyia vivyo hivyo huyu ng'ombe, kuhani atawafanyia upatanisho watu nao watasamehewa.
21 Atamchukua huyo ng'ombe nje ya mji na kumteketeza kama alivyomteketeza ng, ombe wa kwanza. Hii ni sadaka ya dhambi kwa ajili ya mkutano.
22 Mtawala akitenda dhambi bila kukusudia kufanya moja ya yale Bwana Mungu wake ameagiza kutotenda, na anajisikia hatia
23 na kama dhambi yake aliyotenda anaifahamu, ataleta dhabihu yake mbuzi mme asiye na kasoro.
24 Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha mbuzi na kumchinja mahali ambapo huchinja sadaka ya kuteketezwa mbele za Bwana. Hii ni sadaka ya dhambi.
25 Kuhani atachukua damu ya sadaka ya dhambi kwa kidole chake na kuiweka juu ya pembe za madhabahu kwa dhabihu ya kuteketezwa, na atamwaga damu chini ya madhabahu ya dhabihu ya kuteketezwa.
26 Atateketeza mafuta yote katika madhabahu, kama vile mafuta ya dhabihu ya sadaka ya amani, Kuhani atafanya upatanisho kwa ajili ya mtawala kulingana na dhambi yake, na mtawala atakuwa amesamehewa.
27 Kama yeyote wa watu wa kawaida akitenda dhambi bila kukusudia, kufanya vitu ambavyo Bwana ameagiza kutokufanywa na kama ana hatia,
28 ndipo dhambi yake aliyoitenda ikajulikana kwake, ndipo ataleta mbuzi mke asiyekuwa na kasoro awe dhabihu kwa ajili ya dhambi zake alizotenda.
29 Ataweka mikono yake juu ya sadaka ya dhambi na kuchinja sadaka ya dhambi mahali pa sadaka ya kuteketezwa.
30 Kuhani atachukua kiasi cha damu kwa kidole chake na kuweka katika pembe za madhabahu ya dhabihu ya kuteketezwa. Damu yote iliyobaki ataimwaga chini ya madhabahu.
31 Atayaondoa mafuta yote, kama alivyoondoa mafuta katika dhabihu ya amani. Kuhani ataiteketeza katika madhabahu ili kuwa harufu nzuri kwa Bwana. Kuhani atafanya upatanisho kwa mtu, na atasamehewa.
32 Kama mtu ataleta mwanakondoo kama dhabihu yake kwa sadaka ya dhambi, ataleta jike asiye na kasoro.
33 Ataweka mikono kichwani mwa sadaka ya dhambi na atamchinja kuwa sadaka ya dhambi mahali wanapochinjwa sadaka ya kuteketezwa.
34 Kuhani atachukua baadhi ya damu ya sadaka ya dhambi kwa kidole chake na kuweka katika pembe za madhabahu kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, na ataimwaga damu yote chini ya madhabahu.
35 Ataondoa mafuta yote, kama akatavyo mafuta ya mwanakondoo dhabihu ya sadaka ya amani na kuhani ataiteketeza juu ya madhabahu juu ya sadaka ya Bwana itolewayo kwa moto. Kuhani ataleta upatanisho kwa dhambi aliyoifanya, naye atasamehewa.
Mambo ya Walawi 4 in Biblia ya Kiswahili