Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mambo ya Walawi 26:10-23 in Swahili (individual language)

Help us?

Mambo ya Walawi 26:10-23 in Biblia ya Kiswahili

10 Mtakula chakula kilichotunzwa ghalani kwa muda mrefu. Mtayaondoa mazao yaliyohifadhiwa ghalani kwa sababu mtahitaji ghala kwa ajili ya mavuno mapya.
11 Nitaliweka hema langu katikati yenu, nami stachukizwa nanyi.
12 Nitatembea miongoni mwenu nami nitakuwa Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu.
13 Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu, aliyewaleta nyinyi kutoka nchi ya Misri, ili kwamba msingeendelea kuwa watumwa wao. Nimevunja makomeo ya nira yenu na nikawafanya mtembee kwa kunyooka.
14 Lakini ikiwa hamtanisikiliza mimi,
15 na kutozitii amri hizi, na ikiwa mtayakataa maagizo yangu, na kuzichukia sana sheria zangu, kiasi kwamba hamtaweza kuzitii amri zangu zote, lakini mkalivunja agano langu—
16 —kama mtafanya mambo haya, Nami nitafanya hili kwenu: Nitasababisha hofu juu yenu, maradhi na homa kali itakayoangamiza macho na kuondoa uhai wenu. Mtapanda mbegu zenu kwa hasara, kwa sababu adui zenu watakula mazao yake.
17 Nitakaza uso wangu dhidi yenu, na mtashindwa na adui zenu. Watu wanaowachukia watatawala juu yenu, na mtakimbia hata kama hakutakuwa na yeyote anayewafukuza.
18 Iwapo hamtasikiliza maagizo yangu, Nami niwataadhibu vikali mara saba kwa dhambi zenu.
19 Nami nitakivunja kiburi chenu katika uwezo wenu. Nitaifanya mbingu juu yenu iwe kama chuma na nchi yenu kama shaba.
20 Nguvu yenu itatumika bure, kwa sababu nchi yenu haitazalisha mavuno yake, na miti yenu katika nchi haitazaa matunda yake.
21 Iwapo mtataenenda kinyume changu na hamtanisikiliza mimi, nitaleta mapigo mara saba zaidi juu yenu, sawasawa na dhambi zenu.
22 Nitatuma wanyama mapori hatari dhidi yenu, ambao watawaibia watoto wenu, kuangamiza mifugo yenu na kuwafanya mwe wachache katika idadi yenu. Hivyo barabara zenu zitakuwa nyeupe.
23 Endapo pamoja na mambo haya kuwapata lakini msiyakubali marekebisho yangu na mkazidi kuenenda katika upinzani dhidi yangu,
Mambo ya Walawi 26 in Biblia ya Kiswahili