Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mambo ya Walawi 25:5-18 in Swahili (individual language)

Help us?

Mambo ya Walawi 25:5-18 in Biblia ya Kiswahili

5 Hamtasimamia mavuno yoyote ya mazao ya mizabibu iliyojiotesha yenyewe katika mashamba yenu ya mizabibu isiyokatiwa matawi. Huu utakuwa mwaka wa pumziko lenye utulivu kwa ardhi.
6 Chochote ardhi isiyofanyiwa kazi itakachotoa wakati wa Sabato ndicho kitakuwa chakula chako. Wewe mwenyewe, watumwa wako wa kiume na wa kike, watumishi wako wa kuajiriwa na wageni wanaoishi pamoja nawe mnaweza kujikusanyia chakula.
7 Na wnyama wako wa kufugwa na wanyama pori waweze kula chochote ardhi itoacho.
8 Ni lazima kwenu kuhesabu Sabato saba za miaka, yaani, saba mara miaka saba, ikifanya jumla ya miaka arobaini na tisa.
9 Kisha mtapiga sauti ya tarumbeta kila mahali katika siku ya kumi ya mwezi wa saba. Katika Siku ya Upatanisho ni lazima mtapiga tarumbeta katika nchi yenu yote.
10 Nanyi mtautenga mwaka wa hamsini kwa ajili ya Yahweh na mtatangaza uhuru katika nchi yote kwa wakazi wote. Kutakuwa na Yubile kwa ajili yenu, ambayo kwayo mali na watumwa ni lazima warejeshwe kwa familia zao.
11 Mwaka wa saba kutakuwa na Yubile kwenu. Hamtapanda wala kusimamia mavuno ya kijioteshacho chenyewe, na kukusanya kichipukacho kwenye mizabibu isiyokatiwa matawi.
12 Kwa sababu hiyo ni Yubile takatifu kwenu. Nanyi mtakula mazao yanayokua yenyewe kutoka mashambani.
13 Ni lazima muwarejeshe kila mmoja kwenye miliki yake katika mwaka huu wa Yubile.
14 Iwapo utauza ardhi yoyote ya jirani yako au kununua ardhi yake, ni shrti msipunjane au kutendeana kwa hila.
15 Iwapo unanunua ardhi kutoka kwa jirani yako, zingatia idadi ya miaka na mazao ambayo yaweza kuvunwa mpaka mwaka wa Yubile nyingine. Jirani yako anayeuza ardhi ni lazima aihesabu miaka hiyo pia.
16 Miaka inapoongezeka mpaka Yubile nyingine, ataongeza thamani ya ardhi, na miaka inapokuwa michache kufikia Yubile nyingine atashusha thamani, kwa sababu idadi ya mavuno inahusiana na idadi ya miaka kabla ya Yubile nyingine.
17 Msipunjane au kutendeana kwa hila, badala yake, yawapasa kumheshi Yahweh Mungu wenu.
18 Kwa hiyo basi, ni lazima muyatii maagiza, kuzitunza sheria zangu na kuzitekeleza. Nanyi mtaishi katika nchi katika usalama.
Mambo ya Walawi 25 in Biblia ya Kiswahili