Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mambo ya Walawi 25:31-52 in Swahili (individual language)

Help us?

Mambo ya Walawi 25:31-52 in Biblia ya Kiswahili

31 Lakini nyumba za vijijini zisizokuwa na ukuta kuzizunguuka, zitahesabiwa kuwa shamba la nchi. Zaweza kukombolewa, na ni lazima zirejeshwe katika mwaka wa Yubile.
32 Hata hivyo, nyumba zinazomilikiwa na makuhani katika miji yao zaweza kukombelewa wakati wowote.
33 Iwapo mmoja wa makuhani haikombowi nyumba iliyozwa, kisha nyumba hiyo iliyouzwa katika miji ilimo, ni lazima irejeshwe katika mwaka wa Yubile, kwa kuwa nyumba za miji ya makuhani ni mali yao miongoni mwa watu wa Israeli.
34 Lakini yale mashamba yanayozunguka miji yao hayataweza kuuzwa kwa sababu hiyo ni mali ya kudumu ya Makuhani.
35 Ikiwa mwananchi mwenzako anakuwa masikini, kiasi kwamba hawezi kujihudumia, nawe utalazimika kumsaidia kama vile ungemsaidia mgeni au mwingine yeyote kutoka nje aishie miongoni mwenu.
36 Usimtoze riba au kujaribu kunufaika kutoka kwake katika njia yoyote, bali mheshimu Mungu wako ili kwamba ndugu yako aendelee kuishi nawe.
37 Hutampa mkopo wa fedha na kumtoza riba, wala hutamuuzia chakula chako ili kupata faida.
38 Mimi ndimi Yahweh Mungu wako, aliye kuleta wewe kutoka nchi ya Misri, ili kwamba Nikupe nchi ya Kanaani, na kwamba niwe Mungu wako.
39 Iwapo mwananchi mwenzako atakuwa masikini na kujiuza mwenyewe kwako, hutamfanyisha kazi kama mtumwa.
40 Mtendee kama mtumishi wa kuajiriwa. Ni lazima awe kama yule ahudumuye nawe kwa muda mpaka mwaka wa Yubile.
41 Kisha ataondoka kwako, yeye mwenyewe na watoto wake pamoja naye, na atarejea kwenye familia yake mwenyewe na kwenye miliki ya baba yake.
42 Kwa sababu wao ni watumishi wangu niliowaleta kutoka katika nchi ya Misri. Hawatauzwa kama watumwa.
43 Usitawale juu yao kwa ukatili, bali yakupasa kumheshimu Mungu wako.
44 Kwa upande wa watumwa wako wakiume na watumwa wako wa kike, unaowezao kuwapata kutok kwa mataifa yanayokuzunguka, waweza kununua watumwa kutoka kwao.
45 Unaweza pia kununua watumwa kutoka kwa wageni wanaoishi miongoni mwenu, yaani, kutoka familia zao waliopamoja nawe, wale wtoto waliozaliwa katika nchi yako. Wanaweza kuwa mali yako.
46 Unaweza kuzalisha watumwa hao kama urithi kwa watoto wako baada yako, ili kuwamiliki kama mali. Kutoka kwao waweza kununua watumwa daima, lakini hamtawezi kutawala kwa ukali juu ya ndugu zenu walio miogoni mwa watu wa Israeli.
47 Iwapo mgeni anayeishi nawe kwa muda anakuwa tajiri, na ikiwa mmoja wa Waisraeli amekuwa masikini na kujuza mwenyewe kwa familia ya mgeni, au kwa mtu fulani katika familia,
48 baada ya Mwisraeli mwenzako kuwa amenunuliwa. Anaweza kurejeshwa kwa maliopo. Iwapo anaweza kurejeshwa. Mtu fulani katika familia yake anaweza kumkomboa.
49 Anaweza kuwa mjomba wake, au mjomba wa mwanawe, anayemkomboa yeye, au yeyote aliye ndugu yake wa karibu kutoka kwa ukoo wake. Au, iwapo ni mwenye mafanikio, anaweza kujikomboa mwenyewe.
50 Ni lazima apatane na mtu aliyemnunua, itawapasa kuhesabu miaka tangu mwaka aliojiuza kwa mnunuzi wake mpaka mwaka wa Yubile. Ile thamani ya ukombozi wake ihesabiwe kulingana na kiwango cha mshahara anaolipwa mtumishi aliyeajiriwa, kwa idadi ya miaka ambayo angeweza kuendelea kufanya kazi kwa yule aliyemnunua.
51 Endapo kutakuwa kungali na miaka mingi iliyobaki mpaka mwaka wa Yubile, atalazimika kulipa fungu kubwa la fedha kwa ajili ya ukombozi ambao ni uwino wa idadi ya miaka hiyo.
52 Iwapo kuna miaka michache tu iliyobaki mpaka mwaka wa Yubile, atapatana na aliyemnunua ili kuipitia idadi ya miaka iliyobaki mpaka Yubile, naye atalazimika kulipia ukombozi wake kulingana na idadi ya miaka.
Mambo ya Walawi 25 in Biblia ya Kiswahili