Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mambo ya Walawi 25:25-31 in Swahili (individual language)

Help us?

Mambo ya Walawi 25:25-31 in Biblia ya Kiswahili

25 Iwapo Mwisraeli mwenzako anakuwa masikini na kwa sababu hiyo anauza baadhi ya miliki yake, kisha jamaa yake wa karibu anaweza kuja na kuikomboa hiyo miliki ambayo jamaa yake kaiuza kwako.
26 Iwapo mtu hana jamaa wa kuikomboa mali yake, lakini ikiwa kafanikiwa na anao uwezo wa kuikomboa,
27 kisha atahesabu miaka tangu ardhi hiyo ilipouzwa na kurejesha kwa mtu aliyemuuzia fedha iliyosalia. Naye anaweza kuerejea kwenye miliki yake mwenyewe.
28 Lakini ikiwa hawezi kuirejesha kwake ardhi aliyoiuza, nayo hiyo ardhi aliyoiuza itabaki katika umiliki wa yule aliyeinunua mpaka mwaka wa Yubile. Kwenye mwaka wa Yubile, ardhi itarejeshwa kwa mtu aliyeiuza, naye mmiliki wa asili atarejea kwenye mali yake.
29 Ikiwa mtu anauza nyumba iliyo kwenye mji uliozungushiwa ukuta, naye anaweza kuinunua tena ndani ya mwaka baada ya kuuzwa. kwa kuwa, kwa mwaka mzima atakuwa na haki ya ukombozi.
30 Kama nyumba hiyo haitakombolewa kabla ya mwaka mzima, ndipo hiyo nyumba iliyoko kwenye mji uliozungushiwa ukuta itakuwa mali ya kudumu ya yule aliyeinunua, katika vizazi vyote vya uzao wake. Nyumba hiyo haitakuwa ya kurejeshwa katika mwaka wa Yubile.
31 Lakini nyumba za vijijini zisizokuwa na ukuta kuzizunguuka, zitahesabiwa kuwa shamba la nchi. Zaweza kukombolewa, na ni lazima zirejeshwe katika mwaka wa Yubile.
Mambo ya Walawi 25 in Biblia ya Kiswahili