Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mambo ya Walawi 25:1-9 in Swahili (individual language)

Help us?

Mambo ya Walawi 25:1-9 in Biblia ya Kiswahili

1 Yahweh akazungumza na Musa kwenye Mlima wa Sinai, akisema,
2 “Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, “Mtakapoingia katika nchi ambayo ninawapa, kisha hiyo nchi lazima ifanywe iwe ya kuishika Sabato kwa ajili ya Yahweh.
3 Ni lazima mtapanda mazao yenu kwa miaka sita, na kwa miaka sita mtaikatia matawi mizabibu yenu na kukusanya mazao yake.
4 Lakini katika mwaka wa saba, Sabato ya pumziko la utulivu kwa nchi itashikwa, ni Sabato kwa Yahweh. Hamtapanda mashamba yenu wala kuikatia mizabibu yenu matawi yake.
5 Hamtasimamia mavuno yoyote ya mazao ya mizabibu iliyojiotesha yenyewe katika mashamba yenu ya mizabibu isiyokatiwa matawi. Huu utakuwa mwaka wa pumziko lenye utulivu kwa ardhi.
6 Chochote ardhi isiyofanyiwa kazi itakachotoa wakati wa Sabato ndicho kitakuwa chakula chako. Wewe mwenyewe, watumwa wako wa kiume na wa kike, watumishi wako wa kuajiriwa na wageni wanaoishi pamoja nawe mnaweza kujikusanyia chakula.
7 Na wnyama wako wa kufugwa na wanyama pori waweze kula chochote ardhi itoacho.
8 Ni lazima kwenu kuhesabu Sabato saba za miaka, yaani, saba mara miaka saba, ikifanya jumla ya miaka arobaini na tisa.
9 Kisha mtapiga sauti ya tarumbeta kila mahali katika siku ya kumi ya mwezi wa saba. Katika Siku ya Upatanisho ni lazima mtapiga tarumbeta katika nchi yenu yote.
Mambo ya Walawi 25 in Biblia ya Kiswahili