12 Wakamweka kizuizini mpaka Yahweh mwenyewe atakapotangaza mapenzi yake kwao.
13 Kisha Yahweh akamwambia Musa,
14 “Mchukue nje ya kambi huyo aliyemlaani Mungu. Wale wote waliomskia wataweka mikono yao juu ya kichwa chake, na kisha kusanyiko lote watamponda kwa mawe.
15 Ni lazima uwaeleze watu wa Israeli na kusema, 'Yeyote anayemlaani Mungu wake imempasa kubeba hatia yake mwenyewe.
16 Yeye anayelikufuru jina la Yahweh kwa hakika ni lazima auawe. Hakika, kusanyiko lote litampiga mawe, ama awe mgeni au Mwisraeli mwenyeji mzaliwa. Ikiwa yeyote analikufuru jina la Yahweh, ni lazima auawe.
17 Naye amuuaye mtu mwingine ni lazima kwa hakika auewa.
18 Yeye anayemuua mnyama wa mwingine sharti amfidie, uhai kwa uhai.
19 Iwapo mtu anamjeruhi jirani yake, ni lazima atendewe vivyo hivyo alivyomtendea jirani yake:
20 Mvunjiko kwa mvunjiko, jicho kwa jicho, jino kwa jino. Kama amesababisha jeraha kwa mtu, ndivyo ipasavyo kutendwa kwake.
21 Yeyote auaye mnyama ni lazima amfidie, na yeyote auaye mtu ni lazima auawe.
22 Ni lazima mwe na sheria moja kwa wote, mgeni na Mwisraeli mwenyeji mzaliwa, kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh Mungu wanu.”