Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mambo ya Walawi 18:15-28 in Swahili (individual language)

Help us?

Mambo ya Walawi 18:15-28 in Biblia ya Kiswahili

15 Usilale na binti- mkwe wako, Yeye ni mke wa mwanao; usilale naye.
16 Usilale na mke wa kaka yako; usije ukamfedhesha yeye katika njia hii.
17 Usilale na mwanamke kisha na binti yake, au binti wa mwanawe au binti wa binti yake. Hao ni ndugu zake wa karibu, na kulala nao lingekuwa ni uovu.
18 Usimwoe dada ya mke wako kuwa mke wako wa pili na kulala naye wakati bado mke wako wa kwanza angali hai.
19 Usilale na mwanamke wakati wake wa hedhi.
20 Yeye ni najisi kwa wakati huo. Usilale na mke wa jilani yako na kujichafua mwenyewe kwake katika njia hii.
21 Msiwatoe watoto wenu ili kuwapitisha kwenye moto, ili kwamba muwatoe sadaka kwa Moleki, kwa sababu msije mkalinajisi jina la Mungu wenu. Mimi ndimi Yahweh.
22 Usilale na mwanaume mwingine kama ulalavyo na mwanamke. Jambo hili lingekuwa uovu.
23 Usilale na myama yeyote na kujitia unajisi kwake. Haimpasi mwanamke kufikiria kulala na mnyama ye yote. Huo ungekuwa upotovu.
24 Msijichafue wenyewe katika njia hizi, kwa kuwa katika njia hizi mataifa yamechafuliwa, mataifa ambayo Nitayafukuza yatoke kwa ajili yenu.
25 Ni kwa sababu nchi imenajisiwa, hivyo niliiadhibu dhambi yao, nayo nchi ikawatapika wakazi wake
26 Kwa hiyo, yawapasa kuzishika amri zangu na maagiza yangu, na msifanye aina yoyote ya mambo haya ya machukizo, wala Mwisraeli mzaliwa au Mgeni aishie miongoni mwenu.
27 Kwa kuwa ni uovu huu ambao watu wametenda, wale ambao waliishi hapa kabla yenu, na sasa nchi imenajisiwa.
28 Kwa hiyo, muwe waangalifu ili kwamba nchi isiwatapike nyinyi baada ya kuwa mmeinajisi, kama ilivyowatapika wale watu waliokuwako kabla yenu.
Mambo ya Walawi 18 in Biblia ya Kiswahili