Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mambo ya Walawi 17:4-10 in Swahili (individual language)

Help us?

Mambo ya Walawi 17:4-10 in Biblia ya Kiswahili

4 kama hamleti katika ingilio la hema la kukutania ili kumtoa dhabihu kwa Yahweh mbele za hema lake la kukutania, mtu huyo ana hatia ya damu iliyomwagika. Amemwaga damu, na mtu huyo ni sharti akatiliwe mabali kutoka miongoni mwa watu wake.
5 Kusudi la amri hii ni kwamba watu wa Israeli wataleta dhabihu zao kwa Yahweh kwenye ingilio la hema la kukutania, watazileta kwa kuhani ziweze kutolewa kuwa matoleo ya shukrani kwa Yahweh, badala ya kutoa dhabihu hadharani katika shamba.
6 Kuhani atainyunyiza damu juu ya madhabahu ya Yahweh kwenye ingilio la hema la kukutania; atayachoma mafuta yake ili kutoa harufu ya kupendeza mbele za Yahweh.
7 Ni lazima watu wasitoe tena dhabihu zao kwa sanamu za mbuzi, ambazo kwazo hutenda kama makahaba. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa ajili yao katika vizazi vya watu wao vyote.
8 Ni lazima uwaambie, 'Mtu yeyote wa Israeli, au Mgeni yeyote aishiye miongoni mwao, atoweye dhabihu
9 na asiilete kwenye ingilio la hema la kukutania ili kuitoa kwa Yahweh, mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.'
10 Na Mtu yeyote wa Israeli, au yeyote wa Wageni anayeishi miongoni mwao, ambaye hunywa damu; nitamkatilia mbali atoke miongoni mwa watu wake.
Mambo ya Walawi 17 in Biblia ya Kiswahili