Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mambo ya Walawi 16:13-33 in Swahili (individual language)

Help us?

Mambo ya Walawi 16:13-33 in Biblia ya Kiswahili

13 Hapo lazima aweke ubani juu ya moto mbele za Yahwe ili kwamba wingu kutoka kwenye ubani liweze kufunika kifuniko cha agano la imani ya upatanisho. Yeye afanye hivyo ili kwamba asife.
14 Ndipo lazima achukue kiasi cha damu ya ng'ombe na kuinyunyiza kwa kidole chake mbele ya kifuniko cha upatanisho. Lazima anyunyize kiasi cha damu kwa kidole chake mara saba mbele ya kifuniko cha upatanisho.
15 Ndipo lazima aue mbuzi kwaajili ya sadaka ya dhambi ambayo ni kwaajili ya watu na kuileta damu yake ndani kwenye pazi. Hapo lazima aifanyie damu kama alivyofanya kwenye damu ya fahali: lazima ainyunyize juu ya kifuniko cha upatanisho na mbele ya kifunuko cha upatanisho.
16 Yeye lazima afanye upatanisho kwaajili ya mahali patakatifu kwa sababu ya matendo ya unajisi ya watu wa Israeli, na kwa sababu ya uasi na dhambi zao zote. Yeye pia lazima afanye haya kwaajili ya hema ya mkutano, ambapo Yahwe anaishi kati yao, katika uwepo wa matendo yao ya unajisi.
17 Hakuna mtu anayetakiwa kuwepo katika hema ya mkutano wakati Haruni anaingia kufanya upatanisho katika mahali patakatifu pa patakatifu, na mpaka atoke nje na amemaliza kufanya upatanisho kwaajili yake mwenyewe na kwaajili ya familia yake, na kwaajili umati wa Israeli.
18 Yeye lazima aende nje kwenye madhabahu hapo mbele za Yahwe na kufanya upatanisho kwaajili ya hiyo, na lazima achukue kiasi cha damu ya mbuzi na kuiweka juu ya pembe za madhabahu yote kuzunguka.
19 Anatakiwa anyunyize kiasi cha damu juu yake kwa kidole chake mara saba kuitakasa na kuitenga maalumu kwa Yahwe, mbali kutoka matendo ya unajisi wa watu wa Israeli.
20 Atakapo maliza kupatanisha kwaajili ya mahali patakatifu sana, hema la mkutano, na madhabahu, lazima amlete mbuzi aliyehai.
21 Haruni lazima aweke mikono yake yote juu ya kichwa cha mbuzi huyu aliyehai na akiri juu yake maovu yote ya watu wa Israeli, uasi wao wote, dhambi zao zote. Ndipo lazima aweke dhambi hizo juu ya kichwa cha mbuzi na amwachie katika uangalizi wa mtu aliyetari kumwongoza mbuzi huyo porini.
22 Mbuzi lazima abebe juu yake mwenyewe uovu wote kwenda mahali pakiwa. Kule msituni, huyo mtu amwache mbuzi aende huru.
23 Ndipo Haruni anapaswa kwenda tena humo kwenye hema ya mkutano na kuvua mavazi ya kitani ambayo amayavaa kabla hajaenda mahali patakatifu sana, na anatakiwa kuyaacha mavazi hayo pale.
24 Anapaswa aoshe mwili wake kwa maji mahali patakatifu, na avae nguo zake za kawaida; pia lazima atoke nje kutoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya kuteketezwa kwaajili ya wale watu, na kwa njia hii anafanya upatanisho kwaajili yake mwenyewe na kwaajili ya watu.
25 Lazima yeye achome mafuta ya sadaka ya dhambi juu ya madhabahu.
26 Huyu mtu anayemwacha mbuzi msingiziwa aende huru anafua nguo zake na kuosha mwili wake katika maji; baada ya hayo, anaweza kurudi tena kambini.
27 Yule fahali kwaajili ya sadaka ya dhambi na mbuzi kwaajili ya sadaka za dhambi, ambaye damu yake ililetwa kufanya upatanisho katika mahali patakatifu, lazima ipelekwe nje ya kambi. kule lazima wachome, ngozi zao, nyama yao na kinyesi chao.
28 Huyu anayechoma sehemu hizo lazima afue nguo zake na aoge mwili wake katika maji; baada ya hapo, anaweza kurudi tena kwenye kambi.
29 Hii itakuwa sharti kwaajili yenu kwamba katika mwezi wa saba, kwenye siku ya kumi ya mwezi, mtanyenyekea wenyewe na msifanye kazi, iwe mwenyeji wa kuzaliwa au mgeni anayeishi kati yenu.
30 Hii ni kwasababu katika siku hii ya upatanisho utafanywa kwaajili yenu, kuwatakasa ninyi kutoka dhambi zenu zote ili mwe safi mbele za Yahwe.
31 Hii ni maalumu kwa Sabato ya kupumzika kwaajili yenu, na lazima mnyenyekee wenyewe na msifanye kazi. Hili litakuwa sharti kati yenu.
32 Kuhani mkuu, ambaye atapakwa mafuta na kuwekwa wakfu kuwa kuhani mkuu katika nafasi ya baba yake, lazima afanye upatanisho huu na kuvaa mavazi ya kitani, hayo ni mavazi matakatifu.
33 Lazima afanye upatanisho kwaajili ya mahali patakatifu sana; lazima afanye upatanisho kwaajili ya hema ya mkutano na madhabahu, na lazima afanye upatanisho kwaajili ya makuhani na kwaajili ya kusanyiko la watu.
Mambo ya Walawi 16 in Biblia ya Kiswahili