Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mambo ya Walawi 14:16-39 in Swahili (individual language)

Help us?

Mambo ya Walawi 14:16-39 in Biblia ya Kiswahili

16 na kunyunyiza baadhi ya mafuta kwa kidole mara saba mbele za Yahwe.
17 kuhani ataweka mafuta yaliyobaki kwenye mkono wake kwenye ncha ya sikio la kulia la mtu wa kutakaswa, juu ya dole gumba la mkono wa kulia, na katika dole kubwa la mguu wa kulia. Lazima aweke mafuta haya juu ya damu kutoka kwenye sadaka ya hatia.
18 Kama kwa mafuta yaliyosalia kwamba katika mkono wa kuhani, atayaweka juu ya kichwa cha mtu ambaye atakaswaye, na kuhani atafanya utakaso kwaajili yake mbele za Yahwe.
19 Ndipo kuhani atatoa sadaka ya dhambi na kufanya upatanisho kwaajili yake atakaswaye kwa sababu ya kutokuwa safi kwake, na badaye ataua sadaka ya kuchomwa.
20 Ndipo kuhani atatoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya nafaka juu ya madhabahu. Kuhani atafanya upatanisho kwaajili ya mtu huyo, na ndipo atakuwa safi.
21 Kwa namna hiyo, kama mtu ni masikini na hawezi kumudu matoleo haya, ndipo anaweza kuchukua kondoo mmoja dume kama sadaka ya hatia ya kutikiswa, kufanya upatanisho kwaajili yake mwenyewe, na moja ya kumi ya efa ya unga safi uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, na chombo cha mafuta,
22 pamoja na njiwa wawili au kinda mbili za njiwa, ambao anaweza kupata; ndege mmoja atakuwa sadaka ya dhambi na mwingine sadaka ya kuteketezwa.
23 Katika siku ya nane lazima awalete kwa kuhani kwaajili ya utakaso, pakuigilia katika hema ya mkutano, mbele ya Yahwe.
24 Kuhani atachukua mwana kondoo kwaajili ya sadaka, na atachukua pamoja na kiasi cha mafuta ya mzeituni, na ataviinua juu kama anaviwasilisha kwa Yahwe.
25 Atamuua mwana kondoo kwaajili ya sadaka ya hatia, na atachukua baadhi ya ya damu ya sadaka ya hatia na kuiweka juu ya ncha ya sikio la kulia la yule wakutakaswa, juu ya dole gumba la mkono wake wa kulia, na kwenye dole kubwa la mguu, wa kulia.
26 Ndipo kuhani atamimina baadhi ya mafuta katika kiganja cha mkono wake wa kushoto,
27 na atanyunyiza kwa kidole chake cha kulia baadhi ya mafuta ambayo yako kwenye mkono wa kushoto mara saba mbele za Yahwe.
28 Ndipo kuhani ataweka kiasi cha mafuta ambayo yako kwenye mkono wake kwenye ncha ya sikio la yule mtu wa kutakaswa, katika dole gumba lake la mkono wa kulia, na dole kubwa la mguu wa kulia, maeneo yale yale ambayo kaweka damu ya sadaka ya hatia.
29 Ataweka mafuta yaliyobaki yaliyo mkononi mwake juu ya yule wakutakaswa, kufanya upatanisho kwaajili yake mbele za Yahwe.
30 Lazima atoe sadaka ya njiwa au makinda ya njiwa, yale ambayo mtu ameweza kupata -
31 moja kama ya sadaka ya dhambi na nyingine kama sadaka ya kuteketezwa, pamoja na sadaka ya nafaka. Ndipo kuhani atafanya upatanisho kwaajili ya yule ambaye atatakaswa mbele za Yahwe.
32 Hii ni sheria kwaajili ya mtu kwake kuna athari za ugonjwa wa ngozi, ambaye hawezi kumudu kiwango cha sadaka kwaajili ya utakaso wake.”
33 Yahwe alizungumza na Musa na Haruni, akisema,
34 “Wakati mtakuja katika nchi ya Kanaani ambayo nimewapa kama miliki, na kama naweka ukungu unaenea ndani ya nyumba katika nchi ya miliki yenu,
35 ndipo yeye ambaye anamiliki nyumba ile lazima aje na kumwambia kuhani. Lazima aseme 'Inaonekana kwangu kuna kitu fulani kama ukungu ndani ya nyumba yangu.'”
36 Ndipo kuhani ataamuru kwamba watoe vitu vyote ndani kabla hajaenda ndani kuona uthibitisho wa ukungu, kiasi kwamba hakuna ndani ya nyumba kitakachofanywa najisi. Badaye kuhani lazima aende ndani kuona humo ndani.
37 Yeye lazima achunguze ukungu kuona kama umo katika kuta za nyumba, na kuona ikiwa kunaonekana ukijani au wekundu katika bonde za mwonekano wa kuta.
38 Kama nyumba inao ukungu, ndipo kuhani atatoka nje ya nyuma na kufunga mlango wa nyumba kwa siku saba.
39 Ndipo kuhani atarudi tena katika siku ya saba na kuichunguza kuona kama ukungu umeenea katika kuta za nyumba.
Mambo ya Walawi 14 in Biblia ya Kiswahili