Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mambo ya Walawi 13:50-59 in Swahili (individual language)

Help us?

Mambo ya Walawi 13:50-59 in Biblia ya Kiswahili

50 Yapasa kuhani akichunguze hicho kifaa kwa ajili ya ukungu; ni lazima akitenge kitu chochote kilicho na ukungu kwa siku saba.
51 Naye atauchunguza tena huo ukungu katika siku ya saba. Endapo utakuwa umesambaa katika kifaa hicho, basi ni wazi kwamba huo ni ukungu wenye kuangamiza, na hicho kifaa ni najisi.
52 Na mwenye kukimiliki atalazimika kukichoma na kukiteketeza kabisa hicho kifaa kilichoonekana na ukungu ndani yake, haijalishi kiwe ni kifaa cha aina gani, kwani huo ukungu unaweza kusababisha ugonjwa.
53 Iwapo kuhani anakichunguza hicho kifaa na kuona kwamba ukungu haujaenea kwenye vazi au chombo kilichosukwa au kusokotwa kutokana na sufu, kitani au ngozi,
54 basi atawaagiza wakisafishe hicho kifaa kilichopatikana na ukungu, naye yampasa kukitenga kwa siku saba zaidi.
55 Kisha kuhani atakichunguza tena hicho kifaa chenye ukungu baada ya kuwa kimesafinshwa. Kama ukungu haukubadilika rangi yake, hata kama haukusambaa, kifaa hicho ni najisi. Yapasa kichomwe, haijalishi ni wapi ukungu huo utakuwa umekichafua.
56 Iwapo kuhani anakichunguza hicho kifaa, na kama ukungu umefifia baada ya kuwa umeoshwa, basi atakirarua kile kipande kilichochaufuliwa kutoka kwenye vazi au kutoka kwenye ngozi, au kutoka kwenye chombo kilichosukwa au kusokotwa.
57 Ikiwa ukungu unazidi kuonekana katika vazi, ama katika chombo kilichosukwa au kufumwa, au katika kitu chochote kilichotengenezwa kwa ngozi, basi, ukungu utakuwa unasambaa. Kifaa chochote kilicho na ukungu ni lazima kichomwe.
58 Vazi au kitu chochote kilichosukwa au kufumwa kutokana na sufu, au kitani, au ngozi au kitu chochote kilichotengenezwa kwa ngozi—iwapo unakisafisha kifaa nao ukungu ukawa umetoka, nacho kifaa lazima kisafishwe mara ya pili, kisha kitakuwa safi.
59 Hii ndiyo sheria ihusuyo ukungu katika vazi la sufu au kitani, au kwenye kitu chochote kilichosukwa au kufumwa kutokana na sufu, au kitani, au kitu chochote kilichotengenewa kwa ngozi, ili kwamba mweze kuvitangaza kuwa safi au najisi.
Mambo ya Walawi 13 in Biblia ya Kiswahili