Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mambo ya Walawi 13:47-55 in Swahili (individual language)

Help us?

Mambo ya Walawi 13:47-55 in Biblia ya Kiswahili

47 Kuna wakati fulani vazi la mtu hupata ukungu juu yake. Laweza kuwa vazi, ama la sufu au kitani,
48 au kitu chochote kilichosukwa au kufumwa kutokana na sufu au kitani, au ngozi au kitu chochote kilichotengenezwa kwa ngozi.
49 Iwapo sehemu iliyochafuliwa ina rangi ya kijani au nyekundu katika vazi, ngozi, kifaa kilichosukwa au kufumwa, basi huo ni ukungu uanasambaa, ni lazima uonyeshwe kwa kuhani.
50 Yapasa kuhani akichunguze hicho kifaa kwa ajili ya ukungu; ni lazima akitenge kitu chochote kilicho na ukungu kwa siku saba.
51 Naye atauchunguza tena huo ukungu katika siku ya saba. Endapo utakuwa umesambaa katika kifaa hicho, basi ni wazi kwamba huo ni ukungu wenye kuangamiza, na hicho kifaa ni najisi.
52 Na mwenye kukimiliki atalazimika kukichoma na kukiteketeza kabisa hicho kifaa kilichoonekana na ukungu ndani yake, haijalishi kiwe ni kifaa cha aina gani, kwani huo ukungu unaweza kusababisha ugonjwa.
53 Iwapo kuhani anakichunguza hicho kifaa na kuona kwamba ukungu haujaenea kwenye vazi au chombo kilichosukwa au kusokotwa kutokana na sufu, kitani au ngozi,
54 basi atawaagiza wakisafishe hicho kifaa kilichopatikana na ukungu, naye yampasa kukitenga kwa siku saba zaidi.
55 Kisha kuhani atakichunguza tena hicho kifaa chenye ukungu baada ya kuwa kimesafinshwa. Kama ukungu haukubadilika rangi yake, hata kama haukusambaa, kifaa hicho ni najisi. Yapasa kichomwe, haijalishi ni wapi ukungu huo utakuwa umekichafua.
Mambo ya Walawi 13 in Biblia ya Kiswahili