Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mambo ya Walawi 13:24-52 in Swahili (individual language)

Help us?

Mambo ya Walawi 13:24-52 in Biblia ya Kiswahili

24 Ngozi inapoungua na nyama mbichi ya inamekuwa na wekundu uliochanganyika na weupe au doa jeupe,
25 kisha kuhani ataichunguza kuona kama malaika zilizoko kwenye doa hilo zimebadilika na kuwa nyeupe, na kama limeonekana kwenda chini zaidi ya ngozi, kama limekuwa hivyo, basi huo ni ugonjwa wa kuambukiza. Umejitokeza kwenye jeraha la moto, naye kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni ugonjwa wa kuambukiza.
26 Lakini endapo kuahani analichunguza na naona kwamba hakuna malaika nyeupe kwenye doa, na kwamba halikuenda chini ya ngozi bali linafifia, basi, kuhani atamtenga mtu huyo kwa siku saba.
27 Kisha yapasa kuahani kumchunguza tena katika siku ya saba. Iwapo litakuwa limesambaa kwa upana kwenye ngozi, naye kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni ugojwa wa kuambukiza.
28 Iwapo hilo doa lisalia mahali pake na halitakuwa limesambaa kwenye ngozi bali limefifia, ni uvimbe tu kutokana na kuungua moto, naye kuhani atamtangaza kuwa safi, kwa kuwa siyo zaidi ya jeraha la kuungua.
29 Iwapo mwanaume au mwanamke ana ugonjwa wa kuambukiza kichwani au kidevuni pake,
30 kisha kuhani atamchunguza mtu huyo kwa ajili ya ugonjwa wa kuambukiza ili kuona kama unakwenda ndani zaidi ya ngozi, na kama kuna nywele za manjano, nyembamba ndani yake. endapo zinaonekana, kisha kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni mwasho, ugonjwa wa kuambukiza kichwani au kidevuni.
31 Iwapo kuhani anachunguza ugonjwa wa mwasho na anagundu kuwa hauko chini ya ngozi, na kama hakuna nywele nyeusi ndani yake, kisha kuhani atamtenga mtu huyo mwenye ugonjwa wa mwasho kwa siku saba.
32 Katika siku ya saba kuhani atauchunguza tena huo ugonjwa ili kuona kama umesambaa, Endapo hakuna malaika za manjano, na iwapo ugonjwa uko usawa ngozi tu,
33 basi, yapasa mtu huyo kunyolewa., lakini sehemu yenye ugonjwa haitanyolewa, naye kuhani atamtenga mtu huyo mwenye ugonjwa wa mwasho kwa siku saba.
34 Katika siku ya saba kuhani atauchunguza tena ugonjwa ili kuona kama umacha kusambaa ndani ya ngozi. Iwapo unaonekana kuwa hukwenda chini zaidi ya ngozi, kisha kuhani atamtangaza kuwa safi. Mtu huyo yapasa kufua nguo zake, na kisha atakuwa safi.
35 Lakini ikiwa ugonjwa wa mwasho umeenea kwa sehemu kubwa kwenye ngozi baada ya kuhani kutangaza kuwa alikuwa safi,
36 naye kuhani itabidi amchunguze tena. Iwapo ugonjwa utakuwa umesambaa katika ngozi, kuhani hahitajiki kutafuta nywele za manjano. Mtu huyo ni najisi.
37 Lakini iwapo katika mtazamo wa kuhani inaonekana kuwa huo ugonjwa wa mwasho umekoma kusambaa, basi huo ugonjwa umekwisha pona. Yeye ni safi, naye kuhani atamtangaza kuwa safi.
38 Iwapo mwanume au mwanamke ana madoa juu ya ngozi,
39 kisha kuhani atamchunguza mtu huyo ili kuona kama hayo madoa ni meupe kwa kufiifia, ambalo ni kovu tu lililojitokeza kwenye ngozi. Yeye yu safi.
40 Iwapo nywele za mtu zimenyonyoka kichwani, yeye ni kipara lakini yu safi.
41 Na iwapo nywele zake zimenyonyoka upande wa mbele wa kichwa chake, na iwapo paji lake la uso lina kipara, yeye yu safi.
42 Lakini endapo kuna kidonda chenye wekundu uliochanganyika na weupe, juu ya kipara chake au paji lake la uso, huo ni ugonjwa wa kuambukiza uliojitokeza.
43 Naye kuhani atamchunguza ili kuona iwapo uvimbe wa eneo linaugua juu ya upara wake au paji lake la uso lina wekundu uliochanganyika na weupe, kama kuonekana kwa ugonjwa wa kuambukiza kwenye ngozi.
44 Ikionekana hivyo, basi huyo ana ugonjwa wa kuambukiza naye ni najisi. Hakika kuhani atamtangaza kuwa najisi kwa sababu ya ugonjwa wake kichwani pake.
45 Mtu aliye na ugojwa wa kuambukiza atavaa nguo zilizochanika, ni lazima nywele zake ziachwe wazi, na yampasa kufunika uso wake mpaka puani na kupiga kelele, 'Najisi, najisi.'
46 Naye atakuwa najisi siku zote za ugonjwa wake wa kuambukiza. Kwa sababu anao ugonjwa unaosambaa, yapasa kuishi peke yake nje ya kambi.
47 Kuna wakati fulani vazi la mtu hupata ukungu juu yake. Laweza kuwa vazi, ama la sufu au kitani,
48 au kitu chochote kilichosukwa au kufumwa kutokana na sufu au kitani, au ngozi au kitu chochote kilichotengenezwa kwa ngozi.
49 Iwapo sehemu iliyochafuliwa ina rangi ya kijani au nyekundu katika vazi, ngozi, kifaa kilichosukwa au kufumwa, basi huo ni ukungu uanasambaa, ni lazima uonyeshwe kwa kuhani.
50 Yapasa kuhani akichunguze hicho kifaa kwa ajili ya ukungu; ni lazima akitenge kitu chochote kilicho na ukungu kwa siku saba.
51 Naye atauchunguza tena huo ukungu katika siku ya saba. Endapo utakuwa umesambaa katika kifaa hicho, basi ni wazi kwamba huo ni ukungu wenye kuangamiza, na hicho kifaa ni najisi.
52 Na mwenye kukimiliki atalazimika kukichoma na kukiteketeza kabisa hicho kifaa kilichoonekana na ukungu ndani yake, haijalishi kiwe ni kifaa cha aina gani, kwani huo ukungu unaweza kusababisha ugonjwa.
Mambo ya Walawi 13 in Biblia ya Kiswahili