Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mambo ya Walawi 13:18-36 in Swahili (individual language)

Help us?

Mambo ya Walawi 13:18-36 in Biblia ya Kiswahili

18 Mtu anapokuwa na jipu juu yangozi yake na limishapona,
19 na mahali pa jipu pamekuwa na uvimbe au doa lenye kung'aa, wekundu unaochanganyikana na weupe, yapasa kuonyeshwa kwa kuhani.
20 Naye kuhani atalichunguza ili kuona kama linaonekana limekwenda chini ya ngozi, na kama hizo malaika zimebadilika kuwa nyeupe, kama ni hivyo, kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni ugonjwa wa kuambukiza, endapo utakuwa umezalishwa mahali lilipokuwa jipu hilo.
21 Lakini endapo kuhani atakuwa amelichunguza na haoni malaika nyeupe ndani yake, na kwamba iliko chini ya ngozi bali limefifia, kisha kuhani atamtenga kwa siku saba.
22 Kama linaenea kwa kupanuka kwenye ngozi, kisha kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni ugonjwa wa kuambukiza.
23 Lakini kama hilo doa lenye kung'ara linabaki mahali pake na halijasambaa, basi hilo ni kovu la jipu, naye kuhani atamtangaza kuwa safi.
24 Ngozi inapoungua na nyama mbichi ya inamekuwa na wekundu uliochanganyika na weupe au doa jeupe,
25 kisha kuhani ataichunguza kuona kama malaika zilizoko kwenye doa hilo zimebadilika na kuwa nyeupe, na kama limeonekana kwenda chini zaidi ya ngozi, kama limekuwa hivyo, basi huo ni ugonjwa wa kuambukiza. Umejitokeza kwenye jeraha la moto, naye kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni ugonjwa wa kuambukiza.
26 Lakini endapo kuahani analichunguza na naona kwamba hakuna malaika nyeupe kwenye doa, na kwamba halikuenda chini ya ngozi bali linafifia, basi, kuhani atamtenga mtu huyo kwa siku saba.
27 Kisha yapasa kuahani kumchunguza tena katika siku ya saba. Iwapo litakuwa limesambaa kwa upana kwenye ngozi, naye kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni ugojwa wa kuambukiza.
28 Iwapo hilo doa lisalia mahali pake na halitakuwa limesambaa kwenye ngozi bali limefifia, ni uvimbe tu kutokana na kuungua moto, naye kuhani atamtangaza kuwa safi, kwa kuwa siyo zaidi ya jeraha la kuungua.
29 Iwapo mwanaume au mwanamke ana ugonjwa wa kuambukiza kichwani au kidevuni pake,
30 kisha kuhani atamchunguza mtu huyo kwa ajili ya ugonjwa wa kuambukiza ili kuona kama unakwenda ndani zaidi ya ngozi, na kama kuna nywele za manjano, nyembamba ndani yake. endapo zinaonekana, kisha kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni mwasho, ugonjwa wa kuambukiza kichwani au kidevuni.
31 Iwapo kuhani anachunguza ugonjwa wa mwasho na anagundu kuwa hauko chini ya ngozi, na kama hakuna nywele nyeusi ndani yake, kisha kuhani atamtenga mtu huyo mwenye ugonjwa wa mwasho kwa siku saba.
32 Katika siku ya saba kuhani atauchunguza tena huo ugonjwa ili kuona kama umesambaa, Endapo hakuna malaika za manjano, na iwapo ugonjwa uko usawa ngozi tu,
33 basi, yapasa mtu huyo kunyolewa., lakini sehemu yenye ugonjwa haitanyolewa, naye kuhani atamtenga mtu huyo mwenye ugonjwa wa mwasho kwa siku saba.
34 Katika siku ya saba kuhani atauchunguza tena ugonjwa ili kuona kama umacha kusambaa ndani ya ngozi. Iwapo unaonekana kuwa hukwenda chini zaidi ya ngozi, kisha kuhani atamtangaza kuwa safi. Mtu huyo yapasa kufua nguo zake, na kisha atakuwa safi.
35 Lakini ikiwa ugonjwa wa mwasho umeenea kwa sehemu kubwa kwenye ngozi baada ya kuhani kutangaza kuwa alikuwa safi,
36 naye kuhani itabidi amchunguze tena. Iwapo ugonjwa utakuwa umesambaa katika ngozi, kuhani hahitajiki kutafuta nywele za manjano. Mtu huyo ni najisi.
Mambo ya Walawi 13 in Biblia ya Kiswahili