Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mambo ya Walawi 13:12-18 in Swahili (individual language)

Help us?

Mambo ya Walawi 13:12-18 in Biblia ya Kiswahili

12 Iwapo huo ugonjwa unajitokeza na kupanuka zaidi kwenye ngozi, na kuifunika ngozi ya mtu kwa ugonjwa tangu kichwani pake hata miguuni, maadamu anajitokeza kwa kuhani,
13 naye kuhani atamchunguza ili kuona kama huo ugonjwa umeshaenea mwili wake wote. Ikiwa imetokeo hivyo, kuhani atamtangaza mtu huyo aliye na ugonjwa kuwa ni safi. Ikiwa amebadilika kuwa mweupe, huyo ni safi.
14 Lakini ikiwa nyama mbichi imeonekana juu yake, atakuwa najisi.
15 Kuhani ataiangalia hiyo nyama mbichi na kumtanga kuwa najisi kwa sababu hiyo nyama mbichi ni najisi. Huo ni ugonjwa wa kuambukiza.
16 Lakini endapo hiyo nyama mbichi inageuka kuwa nyeupe tena, naye huyo mtu hana budi kwenda kwa kuhani.
17 Kuhani atamchunguza ili kuona kama hiyo nyama imebadilika kuwa nyeupe. Kama imekuwa hivyo naye kuhani atatangaza kwamba mtu huyo kuwa ni safi.
18 Mtu anapokuwa na jipu juu yangozi yake na limishapona,
Mambo ya Walawi 13 in Biblia ya Kiswahili