Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mambo ya Walawi 10:3-12 in Swahili (individual language)

Help us?

Mambo ya Walawi 10:3-12 in Biblia ya Kiswahili

3 Kisha Musa akamwambia Aroni, Hivi ndiyo Yahweh alivyokuwa akizunguzia aliposema, 'Nitaufunua utakatifu wangu kwa wale wajao mbele zangu. Nami nitatukuzwa mbele za watu wote.'” Naye Aroni hakusema neno lolote.
4 Musa akamwita Mishaeli na Elzafani, wana wa Uzieli mjomba wa Aroni, naye akamwambia, “njoo huku na uwatowe ndugu zako nje ya kambi watoke mbele ya hema.”
5 Hivyo wakakaribia na kuwachukua wangali wamevaa kanzu zao za kikuhani, nao wakawapeleka nje ya kambi, kama Musa alivyokuwa ameelekeza. Kisha Musa akamwambia Aroni na wanawe wengine wawili, Eliezari na Ithamari,
6 Msiache wazi nywele za vichwa vyenu, wala msirarue nguo zenu, ili kwamba msije mkafa, na kwamba Yahweh asilikasirikie kusanyiko zima. Lakini waacheni jamaa zenu, nyumba yote ya Israeli waweze kufanya ibada za maombolezo kwa ajili ya hao ambao Yahweh amewaangamiza kwa moto.
7 Msiende nje kutoka kwenye ingilio la hema la kukutania, ama sivyo mtakufa, kwa kuwa mafuta ya Yahweh ya upako yako juu yenu.” Kwa hiyo wakatenda sawasawa na maelekezo ya Musa.
8 Mungu akazungumza na Aroni, akisema,
9 “Msinywe mvinyo wala kinywaji kikali, wewe, au wanao wanaobaki pamoja nawe, ili kwamba mtakapoingia kwenye hema ya kukutania msije mkafa. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu,
10 ili kupaambanua kati ya mambo matakatifu na mambo ya kawaida, na kati ya najisi na safi,
11 ili kwamba mweze kuwafundisha watu wa Israeli amri zote ambazo Yahweh ameziamru kwa kinywa cha Musa.
12 Musa akazungumza na Aroni na wanawe wawili waliosalia; Eliazari naIthamari, Twaeni sadaka ya nafaka inayobaki kutokana na sadaka ifanywayo kwa Yahweh kwa moto, nanyi ileni kando ya madhabahu bila hamiara, kwa kuwa ni takatifu sana.
Mambo ya Walawi 10 in Biblia ya Kiswahili