Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Hesabu 22:21-33 in Swahili (individual language)

Help us?

Hesabu 22:21-33 in Biblia ya Kiswahili

21 Balaamu akainuka asubuhi, akatandika punda wake, akaenda pamoja na viongozi wa Moabu.
22 Lakini kwa sababu alienda, hasira za Mungu zikawaka. Malaika wa BWANA akasimama barabarani kama adui wa Balaamu, aliyekuwa akimpanda yule punda. Watumishi wawili wa Balaamu walikuwa pamoja naye.
23 Yule punda alimwona yule malaika wa BWANA akiwa amesimama barabarani akiwa na upanga mkononi mwake. Yule punda akageuka na kwenda shambani. Balaamu akampiga yule punda ili arudi barabarani.
24 Sasa malaika wa BWANA akasimama kwenye njia nyembamba katikati ya mashamba ya mizabibu, na kushoto kwake kulikuwa na ukuta.
25 Yule punda akamwona yule malaika wa BWANA tena. Akasogea zaidi ukutani na kuubana mguu wa Balaamu ukutani. Balaamu akampiga tena yule punda.
26 Yule malaika wa BWANA akasogea mbele zaidi kwenye eneo jingine jembamba zaidi ambalo haikuwezekana kugeuka upande mwingine.
27 Yule Punda akamwona tena yule malaika wa BWANA, akalala chini ya Balaamu. Hasira za Balaamu zikawaka, akampiga yule punda kwa fimbo yake.
28 Kisha BWANA akafungua kinywa cha punda na akaongea. Akamwambia Balaamu, “Nimekukosea nini kiasi kwamba umenipiga mara tatu?”
29 Balaamu akamjibu yule punda, “Ni kwa sababu umenitendea kwa ujinga. Natamani kama ningekuwa na upanga mkononi mwangu, kama ningekuwa nao, sasa hivi ningekuwa nimekuua.”
30 Yule punda akamwambia Balaamu, “Je, mimi si punda wako ambaye umenipanda maishani mwako mwote mpaka hivi sasa? Je, nimewahi kuwa na tabia ya kukufanyia hivi hapo awali?” Balaamu akasema “hapana.”
31 Basi BWANA akafungua macho ya Balaamu, na akamwona malaika wa BWANA amesimama barabarani akiwa na upanga mkononi mwake. Balaamu akainamisha kichwa chake chini.
32 Yule malaika wa BWANA akamwambia, “Kwa nini umempiga punda wako mara tatu? Tazama, Nimekuja kama adui yako kwa sababu matendo yako kwangu yamekuwa maovu.
33 Yule punda aliniona na akageuka kutoka kwangu mara tatu. Kama asingekuwa amegeuka kutoka kwangu, hakika ningekuwa nimekua na yeye kumwacha hai.
Hesabu 22 in Biblia ya Kiswahili