Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Hesabu 22:14-27 in Swahili (individual language)

Help us?

Hesabu 22:14-27 in Biblia ya Kiswahili

14 Kwa hiyo wale viongozi wa Moabu wakaondoka na kurudi kwa Balaki. Wakamwambia, “Balaamu amekataa kuambatana nasi.”
15 Balaki akatuma viongozi wengine waliokuwa wanaheshimiwa zaidi kuliko kundi lile la awali.
16 Wakaja kwa Balaamu na kumwambia, “Balaki mwana wa Zippori anasema hivi, 'Tafadhali hebu kitu chochote kisikuzuie kuja kwangu,
17 kwa sababu nitakulipa malipo mazuri sana na kukupa heshima kubwa, nami nitakufanyia chochote utakachoniambia. Tafadhali sana uje unilaanie hawa watu.'”
18 Balaamu akawajibu watu wa Balaki akawaambia, “Hata kama Balaki atanipa ikulu yake ikiwa imejaa fedha na dhahabu, sitaweza kufanya dhidi ya maneno ya BWANA, Mungu wangu na kufanya pungufu au zaidi ya kile anachoniambia.
19 Sasa basi, tafadhali subirini hapa usiku wa leo pia, ili kwamba nipate kujifunza kitu zaidi ambacho BWANA ananiambia.”
20 BWANA akaja kwa Balaamu usiku ule na kumwambia, “kwa kuwa hawa watu wamekuja kukuita, inuka uende nao. Lakini utafanya tu kile nitakachokuambia kufanya.”
21 Balaamu akainuka asubuhi, akatandika punda wake, akaenda pamoja na viongozi wa Moabu.
22 Lakini kwa sababu alienda, hasira za Mungu zikawaka. Malaika wa BWANA akasimama barabarani kama adui wa Balaamu, aliyekuwa akimpanda yule punda. Watumishi wawili wa Balaamu walikuwa pamoja naye.
23 Yule punda alimwona yule malaika wa BWANA akiwa amesimama barabarani akiwa na upanga mkononi mwake. Yule punda akageuka na kwenda shambani. Balaamu akampiga yule punda ili arudi barabarani.
24 Sasa malaika wa BWANA akasimama kwenye njia nyembamba katikati ya mashamba ya mizabibu, na kushoto kwake kulikuwa na ukuta.
25 Yule punda akamwona yule malaika wa BWANA tena. Akasogea zaidi ukutani na kuubana mguu wa Balaamu ukutani. Balaamu akampiga tena yule punda.
26 Yule malaika wa BWANA akasogea mbele zaidi kwenye eneo jingine jembamba zaidi ambalo haikuwezekana kugeuka upande mwingine.
27 Yule Punda akamwona tena yule malaika wa BWANA, akalala chini ya Balaamu. Hasira za Balaamu zikawaka, akampiga yule punda kwa fimbo yake.
Hesabu 22 in Biblia ya Kiswahili