Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Hesabu 1:20-53 in Swahili (individual language)

Help us?

Hesabu 1:20-53 in Biblia ya Kiswahili

20 Kutoka uzao wa Reubeni, mtoto wa kwanza wa Israel, yalihesabiwa majina yote ya kila mwanamume mwenye umri wa miaka ishirini na zaidi wenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka hesabu ya ukoo na familia.
21 Waliwahesabu wanaume 46, 000 kutoka ukoo wa Reubeni.
22 Kutoka uzao wa Simeoni yalihesabiwa majina yote ya kila mwanamume mwenye umri wa miaka ishirini na zaidi au wenye uwezo wa kwenda vitani, kutokana na hesabu ya ukoo na familia.
23 Walihesabu wanaume 59, 300 kutoka kabila la Simeoni.
24 Kutoka uzao wa Gadi yalihesabiwa majina yote ya kila mwanamume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na wenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia.
25 Walihesabu wanaume 45, 650 kutoka kabila la Gadi.
26 Kutoka uzao wa Yuda yalihesabiwa majina yote ya wanaume wenye umri wa miaka ishirini au zaidi na wenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia.
27 walihesabiwa wanume 74, 000 kutoka kabila la Yuda.
28 Kutoka uzao wa Isakari yalihesabiwa majina yote ya kila mwanamume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na wenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia.
29 Walihesabiwa wanaume 54, 000 kutoka kabila la Isakari.
30 Kutoka uzao wa Zabuloni yalihesabiwa majina yote ya kila mwanamume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na wenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia.
31 Walihesabiwa wanume 57, 400 kutoka kabila la Zabuloni.
32 Kutoka uzao wa Efraimu mwana wa Yusufu yalihesabiwa majina yote ya kila mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na wenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia.
33 Walihesabiwa wanaume 40, 500 kutoka kabila la Efraimu.
34 Kutoka uzao wa Manase mwana wa Yusufu yaliheabiwa majina yote ya kila mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na wenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu y a ukoo na familia.
35 Walihesabiwa wanaume 32, 000 kutoka kabila la Manase.
36 Kutoka uzao wa Benjamini yalihesabiwa majina yote ya kila mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na wenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia.
37 Walihesabiwa wanaume 35, 000 kutoka kabila la Benjamini.
38 Kutoka uzao wa Dani yalihesabiwa majina yote ya kila mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na mwenye uwezo wa kwenda vitani, Kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia.
39 Walihesabiwa wanaume 62, 000 kutoka kabila la Dani.
40 Kutoka uzao wa Asheri yalihesabiwa majina yote ya kila mwanume mwenye umri wa miaka ishirini au zadi na mwenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu y a ukoo na familia.
41 Walihesabiwa wanaume 41, 500 kutoka ukoo wa Asheri.
42 Kutoka ukoo wa Naftali yalihesabiwa majina yote ya kila mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na mwenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia.
43 Walihesabiwa wanaume 53, 400 kutoka kabila la Naftari
44 Musa na Haruni waliwahesabu wanaume wote hawa, pamoja na wale wanaume kumi na wawili waliokuwa wakiongoza yale makabila kumi na mawili ya Israeli.
45 Kwa hiyo wanaume wote wa Israeli wenye umri wa miak ishirini au zaidi, wote wenye uwezo wa kwenda vitani, walihesabiwa kutoka kwenye familia zao.
46 Walihesabu wanaume 603, 550.
47 Lakini wanaume toka uzao wa Lawi hawakuhesabiwa,
48 Kwa sababu BWANA alimwambia Musa,
49 “usiwahesabu wale wa kabila la Lawi wala kuwajumuisha kwenye jumla ya watu wa Israeli.
50 Badala yake, waagize Walawi kuliangalia hema la amri za agano, na kuangalia mapambo ya hema na vyote vilivyomo. Walawi watalazimika kulibeba hema na lazima wayabebe mapambo ya hema. Lazima waliangalie hema na kuyatengeneza mazingira yake. Wataiangalia masikani na kuzitengeneza kambi zinazolizunguka.
51 Kila hema litakapotakiwa kuhamishiwa eneo jingine, Walawi ndio watakaolipeleka pale. Na kila hema litakapotakiwa kusimamishwa, Walawi ndio watakao lisimamisha. Na mgeni yeyote atakayelisogelea hema lazima auawe.
52 Wakati watu wa Israeli watakaposimamisha hema zao, kila mwanaume lazima awe karibu na bango la jeshi lake.
53 Hata hivyo Walawi lazima waweke hema zao kuizunguka hiyo masikani ya amri za agano ili kwamba hasira yangu isije ikawaka juu ya wana wa Israeli. Walawi lazima wailinde hiyo masikani ya amri za agano.”
Hesabu 1 in Biblia ya Kiswahili