Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Hesabu 15:14-39 in Swahili (individual language)

Help us?

Hesabu 15:14-39 in Biblia ya Kiswahili

14 Na kama kuna mgeni anayeishi kati yenu, au yeyote atakayeishi na watu wa vizazi vyenu vyote, lazima atengeneze sadaka iliytoengenezwa kwa moto, ili kutoa harufu nzuri kwa BWANA. Atafanya kama mnavyofanya.
15 Kutakuwa na sheria hiyo hiyo kwa watu wote na kwa mgeni anayeishi kati yenu, sheria ya kudumu kwa watu wote wa uzao wako. Ninyi mlivyo, ndivyo atakavyokuwa mgeni aliyeishi kati yenu. Atafanya kama mnavyofanya mbele ya BWANA.
16 Sheria na amri hiyohiyo ndiyo itakayotumika kwa mgeni anayeishi kati yenu.”
17 Tena BWANA akanena na Musa, akasema,
18 “Nena wana wa Israeli uwaambie, 'mtakapofika katika nchi ninayowapeleka,
19 mtakapokula chakula kinachozalishwa katika nchi hiyo, mtatoa sadaka ya kunipendeza mimi.
20 Kutoka kwenye mikate yenu ya kwanza mtatoa mkate wa kuinuliwa kama sadaka iliyoinuliwa kutoka mahali pa kupuria nafaka. Mtaiinua kwa jinsi hii.
21 Watu wa uzao wako wote wtanitolea sadaka ya kuinuliwa kutoka kwenye unga wenu wa kwanza.
22 Wakati mwingine mtafanya dhambi pasipo kukusudia, Kama hamtatii amri zote hizi ambazo nimemwambia Musa
23 -kila kitu ambacho nimewaamuru kupitia Musa kuanzia siku ambayo nilianza kuwaamuru na kuendelea kwa watu wote wa uzao wako.
24 Kwa swala la dhambi isiyokusudiwa ambayo watu wote hawaijui, basi watu wote watatoa fahari mchanga sadaka ya kuteketezwa ili kufanya harufu nzuri kwa BWANA. Pamoja na haya yote, lazima itengenezwe sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji, kama ilivyoagaizwa katika amri, na beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
25 Kuhani atafanya sadaka upatanisho kwa watu wote wa Israeli. Watasemehewa kwa sababu dhambi haikukusudiwa. Wametoa sadaka yao, sadaka iliyotengenezwa kwa moto kwa ajili yangu. Wameleta sadaka yao kwangu iliyotengenezwa kwa moto. Wameleta sadaka yao ya uovu mbele yangu kwa ajili ya kosa lao.
26 Ndipo watu wote wa Israeli watasamehewa, pia wageni wote wanaoishi kati yao, kwa sababu watu wote walitenda dhambi pasipo kukusudia.
27 Kama mtu atatenda dhambi bila kukusudia, atatoa mbuzi jike wa umri wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
28 Naye kuhani atafanya upatanisho kwa BWANA kwa ajili ya mtu yule aliyefanya dhambi pasipo kukusudia. Yule mtu atasamehewa baada ya upatanisho kufanyika.
29 Mtakuwa na sheria hiyohiyo kwa mtu yeyote anayefanya dhambi hiyo pasipo kukusudia, sheria hiyohiyo hata kwa mzawa wa Isreli na kwa wageni wanaoishi kati yao.
30 Lakini mtu afanyaye chochote kwa KUkusudia, awe mzawa au mgeni, ananikufuru mimi. Huyo mtu ataondolewa kati ya watu wake.
31 Kwa sababu atakuwa amedharau neno langu na amevunja neno amri yangu, mtu huyo ataondolewa kabisa. Dhambi yake itakuwa juu yake.'”
32 Wakati wana wa Israeli walipokuwa katika jangwa, wakamuona mwanamume akikusanya kuni sikiu ya Sabato.
33 Wale waliomwona wakamleta kwa Musa, Haruni na kwa watu wote.
34 Wakamweka kifungoni kwa sababu ilikuwa haijaamuliwa atakachotendewa.
35 Kisha BWANA akanena na Musa, “Yule mwanamume lazima auawe. Watu wote lazima wampige kwa mawe nje ya kambi.”
36 Kwa hiyo watu wote wakamtoa nje ya kambi nao wakampiga kwa mawe mpaka akafa kama vile BWANA alivyokuwa amemwamuru Musa.
37 BWANA akanena na Musa tena, akasema,
38 “Waambie wana wa Israeli na uwaamuru wajifanyie vishada wavining'inize katika mapindo ya mavazi yao, wavining'ineze katika ncha zote kwa nyuzi za rangi ya samawi. Watu wote watafanya hivi kwa watu wote wa kizazi chote.
39 Huu utakuwa ukumbusho maalumu kwenu, kila mtakapovitazama, mtakumbuka amri zangu, na kuzishika ili kwamba msije mkatangatanga katika mioyo na macho yenu na kuwa waasherati wa hayo.
Hesabu 15 in Biblia ya Kiswahili