Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

2 Wafalme 11:2-13 in Swahili (individual language)

Help us?

2 Wafalme 11:2-13 in Biblia ya Kiswahili

2 Lakini Yehosheba, binti wa mfalme Yehoramu na dada wa Ahazia, akamchukua Yoashi mwana wa Ahazia, na kumficha mbali mwa miongoni mwa watoto wa mfalme waliokuwa wameuawa, wakati wote pamoja na mlezi wake; akawaweka kwenye chumba cha kulala. Wakamficha kutoka Athalia kwa hiyo hakuuawa.
3 Alikuwa pamoja na Yehosheba, wamejificha kwenye nyumba ya Yahwe, kwa mda wa miaka sita, wakati Athalia alipotawala juu ya nchi.
4 Katika mwaka wa saba, Yehoyada alituma ujumbe na kuleta maamiri jeshi mamia wa Wakari na wa walinzi, na kuwaleta kwake mwenyewe, ndani ya nyumba ya Yahwe. Akafanya agano pamoja nao, na kuwaapisha kiapo katika nyumba ya Yahwe. Kisha akawaonyesha mtoto wa mfalme.
5 Akawaamuru, akisema, “Hivi ndivyo mnavyotakiwa kufanya. Theluthi yenu mtakaokuja kwenye Sabato mtakuwa mkiiangalia nyumba ya mfalme,
6 na theluthi mtakuwa langoni mwa Suri, na theluthi langoni nyuma ya walinzi.”
7 Makundi mengine mawili ambayo hayatumikii Sabato, Mtayalinda juu ya nyumba ya Yahwe kwa ajili ya mfalme.
8 Ni lazima mumzunguke mfalme, kila mmoja na silaha zake kwenye mkono wake. Yeyote aingiaye ndani ya safu, auwawe. Lazima mkae pamoja na mfalme kila atokapo na kila aingiapo.
9 Hivyo mamia ya maamri jeshi wakatii kila kitu Yehoyada kuhani alichokiamuru. Kila mmoja akachukua watu wake, wale ambao walitakiwa kuja kutumika siku ya hiyo Sabato, na wale ambao wataacha kuitumika kwenye hiyo Sabato; ndipo wakaja kwa Yehoyada kuhani.
10 Kisha Yehoyada yule kuhani akawapa mikuki na ngao mamia wa maamri jeshi ambayo ilikuwa mali ya mfalme Daudi ambayo ilikuwa kwenye nyumba ya Yahwe.
11 Basi walinzi wakasimama, kila mtu na silaha kwenye mkono wake, kutoka upande wa kuume wa hekalu, kwenda upande wa kushoto, karibu na madhabahu ya hekelu, wakimzunguka mfalme.
12 Kisha Yehoyada akamleta nje mtoto wa mfalme Yoashi, na kumvalisha taji la kifalme, na kumpatia mikataba ya agano. Kisha wakamfanya mfalme na kummiminia mafuta. Wakapiga makofi wakisema, “Mfalme na aishi!”
13 Wakati Athalia aliposikia sauti za walinzi na za watu, alikuja kwa wale watu kwenye nyumba ya Yahwe.
2 Wafalme 11 in Biblia ya Kiswahili