Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

1Wafalme 2:6-30 in Swahili (individual language)

Help us?

1Wafalme 2:6-30 in Biblia ya Kiswahili

6 Mshughulikie Yoabu kwa hekima ambayo umejifunza, lakini usiache mvi zake ziingie kaburini kwa amani.
7 Hata hivyo, uonyeshe utu kwa wana wa Barizilai Mgileadi, na uwaache wawe miongoni mwa wale wanaokula mezani kwako, kwa kuwa walikuja kwangu wakati nilipomkimbia ndugu yangu Absalomu.
8 Tazama, Shimei mwana wa Gera yuko pamoja na wewe, Wabenjamini wa Bahurimu, walionilaani kwa laana ya fujo siku niliyoenda kwa Mahanaimu. Shimei alishuka kuja kuniona pale Yorodani, na nikamwapia kwa BWANA, nikisema, 'Sitawaua kwa upanga,'
9 Kwa hiyo sasa usimwache aiepuke adhabu. Wewe ni mwenye hekima, na utajua jinsi itakavyokupasa kumtendea. Utakileta hicho kichwa chenye mvi chini kaburini.”
10 Ndipo Daudi alipolala na mababu zake na alizikwa kwenye mji wa Daudi.
11 Siku ambazo Daudi alitwala Israeli zilikuwani miaka arobaini. Alikuwa ametawala kwa miaka saba kule Hebroni na kwa miaka thelethini na tatu kule Yerusalemu.
12 Kisha Sulemani akaketi kwenye kiti cha enzi cha baba yake Daudi, na utawala wake ulikuwa imara.
13 Kisha Adoniya mwana wa Hagathi alikuja kwa Bathisheba mama wa Sulemani., Naye akamwuliza, “Je, unakuja kwa amani?” Naye akajiibu. “kwa amani.”
14 Kisha akasema, “Nina jambo la kukuambia.” Naye akajibu, “Sema.”
15 Adoniya amesema, “Unajua kuwa ufalme ulikuwa wangu, na kwamba Israeli yote ilikuwa inanitegemea mimi kuwa mfalme. Hata hivyo, ufalme umegeuzwa na umekuwa wa ndugu yangu, kwani ulikuwa wake toka kwa BWANA.
16 Sasa nina ombi moja kwako. Usinikatalie.” Bathisheba akamwambia, “Sema.”
17 Naye akamwambia, “Tafadhali mwambie mfalme Sulemani, kwa kuwa hatakukatalia, ili kwamba anipatie Abishagi Mshunami awe mke wangu.”
18 Bathisheba akamwambia, “Vyema sana, nitamwambia mfalme”
19 Kwa hiyo Bathisheba akaenda kumwambia, mfalme Sulemani kwa niaba ya Adoniya. Mfalme akainuka kumlaki na akapiga magoti mbele yake. Kisha akaa kwenye kiti chake cha enzi na kulikuwa na kiti kingine cha enzi kilicholetwa kwa ajili ya mama wa mfalme. Naye akaa mkono wa kuume wa mfalme.
20 Ndipo alipomwambia, “Napenda kukuomba ombi moja dogo. Usinikalie.” Mfalme, akamjibu, “Mama omba kwa kuwa sitakukatalia.”
21 Naya akamwambia, “Naomba Abishagi Mshunami apewe Adoniya ndugu yako awe mke wake.”
22 Mfalme Sulemani akamjibu mama yake, “Kwa nini unamwombea Adoniya huyo Abishagi Mshunami? Kwa nini usimwombee ufalme pia, kwa kuwa ni ndugu yangu mkubwa? - au kwa Abiathari kuhani, au Yoabu mwana wa Seruya?”
23 Kisha mfalme Sulemani akaapa kwa BWANA, akisema, “Mungu wangu na anifanyie hivyo, na zaidi pia, kama Adoniya hajayasema haya kinyume na maisha yake.
24 Sasa basi kama BWANA aishivyo, ambaye ndiye alinifanya mimi kuwepo na kunipa kiti cha enzi cha Daudi baba yangu, na ambaye amenifanyia nyumba kwa ahadi yake, hakika Adoniya lazima auawe leo.”
25 Kwa hiyo mfalme Sulemani akamtuma Benaya mwana wa Yehoyada naye akamkuta Adoniya na kumwua.
26 Kisha akamwambia Abiathari kuhani, “Nenda kwa Anathothi, kwenye mashamba yako. unastahili kufa, lakini sitakua sasa hivi, kwa sababu ulilbeba sanduku la BWANA mbele ya Daudi baba yangu na kujitabisha kwa namna mbalimbali kama baba yangu alivyopata tabu.”
27 Kwa hiyo Sulemani akamfukuza Abiathari asiwe kuhani wa BWANA, ili kwamba atimilize maneno ya BWANA, aliyokuwa amesema juu ya nyumba ya Eli.
28 Habari hizo zikamfikia Yoabu, Kwani Yoabu alimuunga mkono Adoniya, ingawa hakumuunga mkono Absalomu. Kwa hiyo Yoabu akakimbilia kwenye hema ya BWANA karibu na madhabahu na akabeba pembe za madhabahu.
29 Sulemani alipoambiwa kuwa Yoabu amekimbilia kwenye hema ya BWANA na sasa alikuwa karibu na madhabahu. Ndipo Sulemani alipomtuma Benaya mwana wa Yehoyada, akisema, “Nenda, ukamwue.”
30 Kwa hiyo Benaya akaenda kwenye hema ya BWANA na kumwambia, “Mfalme anasema utoke hemani.” Yoabu akamjibu, “Hapana, Nitafia hapa,” Kwa hiyo Benaya akarudi kwa mfalme, akasema, “Yoabu amesema atafia kwenye madhabahu,”
1Wafalme 2 in Biblia ya Kiswahili