Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

1Wafalme 22:43-47 in Swahili (individual language)

Help us?

1Wafalme 22:43-47 in Biblia ya Kiswahili

43 Akatembea katika njia za Asa, baba yake, hakuziacha; akafanya yaliyokuwa mema mbele ya macho ya BWANA. Lakini bado mahali pa juu palikuwa hapajabomolewa. Watu walikuwa bado wanaendelea kutoa dhabihu na kufukiza uvumba mahali pa juu.
44 Yehoshafati akafanya amani na mfalme wa Israeli.
45 Kwa mambo mengine kuhusiana na Yehoshafati, na nguvu zake alizoonyesha, na jinsi alivyopigana vita, je, hayajaandikwa katika kitabu cha matukio cha wafalme wa Israeli?
46 Aliwaondoa kutoka katka nchi wale makahaba wa kipagani waliokuwa wamebaki katika siku za baba yake Asa.
47 Hapakuwepo mfalme katika Edomu isipokuwa kaimu mtawala.
1Wafalme 22 in Biblia ya Kiswahili