Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

1Wafalme 19:3-6 in Swahili (individual language)

Help us?

1Wafalme 19:3-6 in Biblia ya Kiswahili

3 Eliya aliposikia hayo, akaiinuka na akakimbia kwa ajili ya kuokoa maisha yake akaja mpaka Beerisheba, ambao ni mji wa Yuda, na akamwacha mtumishi wake huko.
4 Lakini yeye mwenyewe akaenda mwendo wa siku moja huko jangwani, akaja akakaa chini ya mti wa mretemu. Akajiombea mwenyewe kufa, akasema, “Sasa yatosha, BWANA, ichukue roho yangu, kwa kuwa mimi si mzuri kuliko mababu zangu waliokufa.”
5 Kwa hiyo akalala chini ya mretemu. Ghafula malaika akamgusa na akamwambia, “Inuka ule.”
6 Eliya akatazama, karibu na kichwa chake kulikuwa na mkate uliokuwa umeokwa kwa mkaa na gudulia la maji. Kwa hiyo akala na kunywa na kulala tena.
1Wafalme 19 in Biblia ya Kiswahili