Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 9

Zaburi 9:2-10

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2Nitafurahi na kushangilia katika wewe; nitaliimbia jina lako, Wewe uliye juu.
3Maadui zangu wanaponirudia, hujikwaa na kuangamia mbele zako.
4Kwa kuwa umenitetea kwa haki; unakaa kwenye kiti chako cha enzi, ukihukumu kwa haki!
5Uliwakemea mataifa; umewaharibu waovu; na kuwa futilia mbali jina lao milele na milele.
6Maadui wamebomoka kama magofu ulipo pindua miji yao. Kumbukumbu yao yote imepotea.
7Bali Yahweh anadumu milele; ameweka kiti chake cha enzi kwa ajili ya haki.
8Naye atauhukumu ulimwengu kwa haki, na atatekeleza hukumu kwa ajili ya mataifa kwa haki.
9Yahweh pia atakuwa ngome kwake aliye onewa, na ngome wakati wa shida.
10Wale wakujuao jina lako wanaamini katika Wewe, kwa ajili yako, Yahweh, usiwaache wale wakutafutao.

Read Zaburi 9Zaburi 9
Compare Zaburi 9:2-10Zaburi 9:2-10