30Ikiwa watoto wake wataziacha sheria zangu na kutokutii amri zangu,
31na kama watazivunja sheria zangu na kutokuzishika amri zangu,
32ndipo nitauadhiu uasi wao kwa fimbo na uovu wao kwa makofi.
33Lakini sitauondoa kwake upendo wangu thabiti wala kutokuwa mwaminifu kwa ahadi yangu.
34Sitavunja agano langu wala kubadilisha maneno ya midomoni mwangu.
35Mara moja na kwa yote, nimeapa kwa utakatifu wangu sitamdanganya Daudi:
36uzao wake utaendelea milele na kiti chake cha enzi kama vile jua mbele yangu.
37Kitaimarishwa milele kama mwezi, shahidi mwaminifu mawinguni.” Selah