Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 89

Zaburi 89:10-49

Help us?
Click on verse(s) to share them!
10Ulimwangamiza Rahabu kama mmoja aliye uliwa. Uliwatawanya adui zako kwa mkono wako wenye nguvu.
11Mbingu ni zako wewe, na nchi pia. Uliiumba dunia na vyote vilivyomo.
12Uliumba kaskazini na kusini. Tabori na Hermoni hulifurahia jina lako.
13una mkono wa uweza na mkono wenye nguvu, na mkono wako wa kuume uko juu.
14Haki na hukumu ni msingi wa kiti chako. Uaminifu wa agano lako na uaminifu huja mbele zako.
15Wamebarikiwa watu wakuabuduo wewe! Yahwe, wanatembea katika nuru ya uso wako.
16Siku zote wanafurahia katika jina lako, na katika haki yako wanakutukuza wewe.
17Wewe ni fahari ya nguvu zao, na kwa nguvu zako tu washindi.
18Maana ngao zetu ni za kwako Yahwe; mfalme wetu ni wa Mtakatifu wa Israeli.
19Muda mrefu uliopita ulizungumza na waaminfu wako katika maono; ulisema, “Nimeweka taji juu ya mwenye nguvu; nimemuinua aliyechaguliwa kutoka kati ya watu.
20Nimemchagua Daudi mtumishi wangu; kwa mafuta yangu matakatifu nimempaka yeye.
21Mkono wangu utamsaidia yeye; mkono wangu utamtia nguvu.
22Hakuna adui atakaye mdanganya; hakuna mwana wa uovu atakaye muonea.
23Nitawaangamiza adui zake mbele yake; nitawaua wale wamchukiao.
24Kweli yangu na uaminifu wa agano vitakuwa pamoja naye; kupitia jina langu atakuwa mshindi.
25Nitaweka mkono wake juu ya bahari na mkono wake wa kuume juu ya mito.
26Yeye ataniita, 'Wewe ni Baba yangu, Mungu wangu, na mwamba wa wokovu wangu.'
27Nitamjalia kuwa kama mzaliwa wangu wa kwanza, aliye inuliwa zaidi juu ya wafalme wa nchi.
28Nitaongeza uaminifu wa agano langu kwake milele; na agano langu pamoja naye litakuwa salama.
29Nitaufanya uzao wake kudumu milele na kiti chake cha enzi kitadumu kama mbingu zilizo juu.
30Ikiwa watoto wake wataziacha sheria zangu na kutokutii amri zangu,
31na kama watazivunja sheria zangu na kutokuzishika amri zangu,
32ndipo nitauadhiu uasi wao kwa fimbo na uovu wao kwa makofi.
33Lakini sitauondoa kwake upendo wangu thabiti wala kutokuwa mwaminifu kwa ahadi yangu.
34Sitavunja agano langu wala kubadilisha maneno ya midomoni mwangu.
35Mara moja na kwa yote, nimeapa kwa utakatifu wangu sitamdanganya Daudi:
36uzao wake utaendelea milele na kiti chake cha enzi kama vile jua mbele yangu.
37Kitaimarishwa milele kama mwezi, shahidi mwaminifu mawinguni.” Selah
38Lakini wewe umemtupa na kumkataa; umemkasirikia mfalme mpakwa mafuta wako.
39Wewe umelikataa agano la mtumishi wako. Umeinajisi taji yake ardhini.
40Umevunja kuta zake zote. Umeharibu ngome yake.
41Wapita njia wote wamemuibia, amekuwa kitu chenye kinyaa kwa majirani zake.
42Umeinua mkono wa kuume wa adui zake; umewafurahisha adui zake wote.
43Umeyageuza makali ya upanga wake. Na hukumfanya asimame awapo vitani.
44Umeimaliza fahari yake; umekitupa ardhini kiti chake cha enzi.
45Umefupisha siku za ujana wake. Umemfunika kwa aibu. Selah
46Mpaka lini, Yahwe? utajificha, milele? Mpaka lini hasira yako itawaka kama moto?
47Oh, fikiria jinsi muda wangu ulivyo mfupi, na ni kwa ajili gani umewaumba wana wote wa wanadamu wasio na manufaa!
48Ni nani aweza kuishi na asife, au atakaye iokoa nafsi yake dhidi ya mkono wa kuzimu? Selah
49Bwana, yako wapi matendo yako ya zamani ya uaminifu wa agano ambayo ulimwapia Daudi katika kweli yako?

Read Zaburi 89Zaburi 89
Compare Zaburi 89:10-49Zaburi 89:10-49