Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 88

Zaburi 88:2-11

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2Sikiliza maombi yangu; utazame kulia kwangu.
3Maana nimejawa taabu, na uhai wangu umefika kuzimuni.
4Watu hunichukulia kama wale waendao chini shimoni; mimi ni mtu asiye na nguvu.
5Nimetelekezwa miongoni mwa wafu; niko kama mfu alalaye katika kaburi, wao ambao wewe huwajari tena kwa sababu wametengwa mbali na nguvu zako.
6Wewe umeniweka katika sehemu ya chini kabisa ya shimo, sehemu yenye giza na kilindini.
7Gadhabu yako yanielemea, na mawimbi yako yote yanatua juu yangu. Selah
8Kwa sababu yako, wale wanijuao wote hunikwepa. Umenifanya wakutisha machoni pao. Nimefungwa na siwezi kutoroka.
9Macho yangu yamefifia kutokana na shida; kila siku nakuita wewe, Yahwe; ninakunyoshea wewe mikono yangu.
10Je! utafanya miujiza kwa ajili ya wafu? Wale waliokufa watafufuka na kukusifu wewe? Selah
11Uaminifu wa agano lako utatangazwa kaburini? au uaminifu wako mahali pa wafu?

Read Zaburi 88Zaburi 88
Compare Zaburi 88:2-11Zaburi 88:2-11