Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 88

Zaburi 88:10-18

Help us?
Click on verse(s) to share them!
10Je! utafanya miujiza kwa ajili ya wafu? Wale waliokufa watafufuka na kukusifu wewe? Selah
11Uaminifu wa agano lako utatangazwa kaburini? au uaminifu wako mahali pa wafu?
12Matendo yako ya ajabu yatajulikana gizani? au haki yako katika mahali pa usahaulifu?
13Lakini ninakulilia wewe, Yahwe; wakati wa asubuhi maombi yangu huja kwako.
14Yahwe, kwa nini unanikataa? Kwa nini unauficha uso wako mbali nami?
15Nimekuwa nikiteswa kila siku na hatihati ya kifo tangu ujana wangu. Nimeteseka dhidi ya hofu yako kuu; ninakata tamaa.
16Matendo yako ya hasira yamepita juu yangu, na matendo yako ya kutisha yameniangamiza.
17Siku zote yananizingira mimi kama maji; yote yamenizunguka mimi.
18Wewe umemuondoa kwangu kila rafiki na anijuaye. Na sasa anijuaye pekee ni giza.

Read Zaburi 88Zaburi 88
Compare Zaburi 88:10-18Zaburi 88:10-18