Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 81

Zaburi 81:6-13

Help us?
Click on verse(s) to share them!
6“Niliutua mzigo kutoka mabegani mwake; mikono yake ilipumzishwa kubeba kikapu.
7Katika dhiki yako uliniita, nami nikakusaidia; nilikujibu kutoka katika wingu jeusi la radi. Nilikujaribu kwenye maji ya Meriba. Selah
8Sikilizeni, watu wangu, nami nitawaonya, Israeli, kama tu ugalinisikiliza!
9Lazima kati yenu kusiwepo na mungu wa kigeni; haupaswi kumwabudu mungu wa kigeni.
10Mimi ni Yahwe niliyekutoa katika nchi ya Misri, fungua sana kinywa chako, nami nitakijaza.
11Lakini watu wangu hawakusikiliza maneno yangu; Israeli hawakunitii.
12Nikawaacha waende katika katika njia yao wenyewe ya ukaidi ili kwamba waweze kufanya kinachoonekana sahihi kwao.
13Oh, laiti watu wangu wangenisikiliza mimi; oh, watu wangu wangelitembea katika njia yangu.

Read Zaburi 81Zaburi 81
Compare Zaburi 81:6-13Zaburi 81:6-13