Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 76

Zaburi 76:1-12

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Mungu amefanya mwenyewe kujulikana katika Yuda; jina lake ni kuu katika Israeli.
2Hema yake iko salemu; makao yake yako yako Sayuni.
3Huko ndiko alivunja mishale ya upinde, ngao, upanga, na silaha zingine za vita. Selah
4Wewe unang'aa sana na huufunua utukufu wako, ushukapo kutoka milimani, ambako uliwauwa mateka.
5Wenye moyo shujaa walitekwa nyara; walilala mauti. Mashujaa wote walikuwa wanyonge.
6Kwa kukemea kwako, ewe Mungu wa Yakobo, wote gari na farasi walilala mauti.
7Wewe, ndiyo wewe, ni wa kuogopwa; ni nani awezaye kusimama mbele yako wakati ukiwa na hasira?
8Kutoka mbinguni wewe uliifanya hukumu yako isikike; nchi iliogopa na ikaa kimya
9wakati wewe, Mungu, ulipoinuka kutekeleza hukumu na kuwaokoa wote wa nchi walio onewa. Selah
10Hakika hukumu ya hasira yako dhidi ya binadamu itakuletea wewe sifa; wewe hujifunga mwenyewe hasira yako iliyo baki.
11Wekeni nadhiri kwa Yahwe Mungu wenu na kuzihifadhi. Nao wote wamzungukao yeye mleteeni zawadi yeye ambaye ni wa kuogopwa.
12Yeye huzikata roho za wakuu; huogopwa na wafalme wa nchi.

Read Zaburi 76Zaburi 76
Compare Zaburi 76:1-12Zaburi 76:1-12