Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 75

Zaburi 75:1-7

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Tunatoa shukrani kwako, Mungu; tunatoa shukrani, maana wewe unaufunua uwepo wako; watu huzungumza kuhusu kazi zako za ajabu.
2Kwa wakati maalum nitahukumu kwa haki.
3Ingawa nchi na wenyeji wote watatikisika katika hofu, ninaifanyia nchi nguzo za kutosha. Selah
4Nilisema kwa wenye kiburi, “Msiwe wenye kiburi,” na kwa waovu, “Msiinue mapembe.
5Msiinue mapembe yenu kwenye marefu; wala msizungumze kwa shingo ya kiburi.”
6Sio kutoka mashariki au magharibi, na wala sio kutoka jangwani ambako kuinuliwa kunakuja.
7Bali Mungu ni muhumkumu; humshusha huyu na kumuinua huyu.

Read Zaburi 75Zaburi 75
Compare Zaburi 75:1-7Zaburi 75:1-7