11Kwa nini umerudisha nyuma mkono wako, mkono wako wa kuume? Utoe mkono wako kwenye mavazi yako na uwaangamize.
12Lakini Mungu amekuwa mfalme wangu tangu enzi, akileta wokovu tuniani.
13Wewe uliigawa bahari; ulishambulia vichwa vya majitu ya kutisha baharini majini.
14Wewe ulishambulia vichwa vya lewiathani; na kumfanya awe chakula cha viumbe hai jangwani.
15Ulizifungulia chemchem na vijito; uliikausha mito itiririkayo.