Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 73

Zaburi 73:15-28

Help us?
Click on verse(s) to share them!
15Kama ningesema, “Ningesema mambo haya,” kumbe nigewasaliti kizazi hiki cha watoto wenu.
16Ingawa nilijaribu kuyaelewa mambo haya, yalikuwa ni magumu sana kwangu.
17Ndipo nilipoingia patakatifu pa Mungu na kuelewa hatma yao.
18Hakika wewe huwaweka penye utelezi; huwaangusha mpaka palipoharibika.
19Jinsi gani wamekuwa ukiwa kwa muda mfupi! Wamefika mwisho nao wamemaliza kwa utisho.
20Wao ni kama ndoto wakati wa mtu kuamka; Bwana, utakapo inuka, utazidharau ndoto zao.
21Maana moyo wangu ulipata uchungu, nami nilijeruhiwa sana.
22Nilikuwa mjinga na sijui neno; nilikuwa kama mnyama tu mbele yako.
23Lakini mimi nipo pamoja nawe daima; umenishika mkono wa kuume.
24Utaniongoza kwa shauri lako na baadaye utanipokea katika utukufu.
25Ni nani niliye naye mbinguni isipokuwa wewe? Hakuna nimtamaniye duniani isipokuwa wewe.
26Mwili wangu na moyo wangu huwa dhaifu, bali Mungu ndiye nguvu ya moyo wangu daima.
27Wale walio mbali nawe wataangamia; utawaangamiza wote wasio waaminifu kwako.
28Lakini mimi, linipasalo kufanya ni kumkaribia Mungu. Nimemfanya Bwana Yahwe kimbilio langu. Nami nitayatangaza matendo yako yote.

Read Zaburi 73Zaburi 73
Compare Zaburi 73:15-28Zaburi 73:15-28