Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 71

Zaburi 71:9-15

Help us?
Click on verse(s) to share them!
9Usinitupe katika siku za miaka ya uzee wangu; usiniache wakati nguvu zangu zitakapoisha.
10Maana adui zangu wanazungumza kuhusu mimi; wale wanao fatilia uhai wangu wanapanga njama pamoja.
11Wao husema, “Mungu amemuacha; mfuateni na mumchukue, maana hakuna yeyote awezaye kumuokoa yeye.”
12Mungu, usiwe mbali nami; Mungu wangu, harakisha kunisaidia mimi.
13Waaibishwe na kuharibiwa, wale walio adui wa uhai wangu; wavishwe laumu na kudharauliwa, wale watafutao kuniumiza.
14Lakini nitakutumainia wewe siku zote na nitakusifu wewe zaidi na zaidi.
15Kinywa changu kitaongea kuhusu haki yako na wokovu wako mchana kutwa, ingawa ziwezi kuzielewa maana ni nyingi mno.

Read Zaburi 71Zaburi 71
Compare Zaburi 71:9-15Zaburi 71:9-15