Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 71

Zaburi 71:15-24

Help us?
Click on verse(s) to share them!
15Kinywa changu kitaongea kuhusu haki yako na wokovu wako mchana kutwa, ingawa ziwezi kuzielewa maana ni nyingi mno.
16Nitakuja na matendo yenye nguvu ya Bwana Yahwe; nitataja haki yako, yako pekee.
17Mungu, tangu ujana wangu wewe umenifundisha; hata sasa ninatangaza matendo yako ya ajabu.
18Hakika, hata niwapo mzee na mvi kichwani, Mungu, usiniache mimi, kama ambavyo nimekuwa nikitanga nguvu yako kwa vizazi vijavyo, na uweza wako kwa yeyote ajaye.
19Pia haki yako, Mungu, iko juu sana; wewe ambaye umefanya mambo makuu, Mungu, ni nani aliye kama wewe?
20Wewe ambaye umetuonesha sisi mateso mengi utatuhuisha tena na utatupandisha tena juu kutoka kwenye kina cha nchi.
21Uiongeze heshima yangu; rudi tena na unifariji.
22Nami pia nitakushukuru kwa kinubi kwa ajili ya uaminifu wako, Mungu wangu; kwako nitaimba sifa kwa kinubi, Mtakatifu wa Israel.
23Midomo yangu itapiga kelele kwa sababu ya furaha wakati nikikuimbia sifa, hata kwa roho yangu, ambayo wewe umeikomboa.
24Ulimi wangu pia utaongea kuhusu haki yangu mchana kutwa; maana wameaibishwa na kuvurugwa, wale waliotafuta kuniumiza.

Read Zaburi 71Zaburi 71
Compare Zaburi 71:15-24Zaburi 71:15-24