Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 71

Zaburi 71:11-17

Help us?
Click on verse(s) to share them!
11Wao husema, “Mungu amemuacha; mfuateni na mumchukue, maana hakuna yeyote awezaye kumuokoa yeye.”
12Mungu, usiwe mbali nami; Mungu wangu, harakisha kunisaidia mimi.
13Waaibishwe na kuharibiwa, wale walio adui wa uhai wangu; wavishwe laumu na kudharauliwa, wale watafutao kuniumiza.
14Lakini nitakutumainia wewe siku zote na nitakusifu wewe zaidi na zaidi.
15Kinywa changu kitaongea kuhusu haki yako na wokovu wako mchana kutwa, ingawa ziwezi kuzielewa maana ni nyingi mno.
16Nitakuja na matendo yenye nguvu ya Bwana Yahwe; nitataja haki yako, yako pekee.
17Mungu, tangu ujana wangu wewe umenifundisha; hata sasa ninatangaza matendo yako ya ajabu.

Read Zaburi 71Zaburi 71
Compare Zaburi 71:11-17Zaburi 71:11-17