Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 70

Zaburi 70:1-5

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Uniokoe, Mungu! Yahwe, njoo haraka na unisaidie mimi.
2Wale wajaribuo kuchukua uhai wangu waaibishwe na kufedheheshwa; warudishwe nyuma na wasiheshimiwe, wale wafurahiao katika maumivu yangu.
3Warudishwe nyuma kwa sababu ya aibu yao, wale wasemao, “Aha, aha.”
4Wale wakutafutao wafurahi na kushangilia katika wewe; wale waupendao wokovu wako siku zote waseme, “Mungu asifiwe.”
5Lakini mimi ni maskini na muhitaji; harakisha kwangu, Mungu; wewe ni msaada wangu nawe huniokoa mimi. Yahwe, usichelewe.

Read Zaburi 70Zaburi 70
Compare Zaburi 70:1-5Zaburi 70:1-5