Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 69

Zaburi 69:3-10

Help us?
Click on verse(s) to share them!
3Nimechoka sana kwa kulia kwangu; koo langu ni kavu; macho yangu yanafifia wakati namngoja Mungu wangu.
4Wale wanichukiao bila sababu wako zaidi ya nywele za kichwa changu; wale ambao wangeweza kuniua, wakiwa adui zangu kwa sababu zisizo sahihi, ni wengi mno; wanalazimisha nirudishe kile ambacho sijaiba.
5Mungu, wewe unaujua ujinga wangu, na dhambi zangu hazifichiki kwako.
6Usiwaache wale wanao kungoja wewe waaibishwe kwa sababu yangu, Bwana Yahwe wa majeshi; usiwaache wale wanaokutafuta wewe wadharauliwe kwa sababu yangu, Mungu wa Israeli.
7Kwa ajili yako nimestahimili lawama; aibu imeufunika uso wangu.
8Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, nisiye fahamika wala kuaminika kwa watoto wa mama yangu.
9Kwa maana bidii ya nyumba yako imenila, na laumu zao wanao kulaumu wewe zimeniangukia mimi.
10Wakati nilipolia na kutokula chakula, walinitukana.

Read Zaburi 69Zaburi 69
Compare Zaburi 69:3-10Zaburi 69:3-10